Uchambuzi Wetu: Blackberry Playbook

 

Sifa vizuri

  • Inakubali mitandao yenye flash, kwa hivyo video na games mpaka liyamba.
  • Inaonekana ni tablet yenye quality, inakamatika vizuri na kweli ni unapata hisia za kiBB
  • Multitasking ni bora kuliko OS zote, apps zinabaki kuwa ‘live’

Udhaifu

  • BB bridge ina maana walengwa ni watumiaji wa simu za BB tu.
  • Apps ni chache mno, yaani karibu na sifuri.

Mwaka 2011 katika Ulimwengu wa gajeti umetabiriwa kuwa ni mwaka wa kompyuta aina ya tablet. Hii ni sahihi kabisa kwani tukiwa tumeugawa mwaka katikati katika mwezi huu wa Juni tayari kuna tablet zaidi ya 100 zilizotolewa.
Barani Ulaya katikati ya mwazi wa kati yaani 15/06/2011, tablet iliyotengenezwa na RIM yaani Blackberry Playbook imeingia maduka ingawa mauzo yameanza siku moja baadae, kama kawaida yetu tumeitia mikononi kuifanyia majaribio kwa lengo la kuichunga, kuichakachua na kuichambua gajeti hii ili tupate kuipa nafasi yake katika uwanja wa tablet. Awali ya yote kuna mambo matatu makubwa juu ya tablet hii:-

  1. Baada ya kuitumia kwa masaa kadhaa, tunachoweza kusema ni kuwa tablet itakayotoa ushindani mzuri kwa baadae, tutaeleza kwa kina ni kwa nini sio sasa hivi bali baadae. 
  2. Ukiondoa iPad 2, ni tablet pekee ya kiwango cha juu ambayo haitumii android OS ya Google, kwa hiyo angalau kuna chaguo la tablet nyingine kama hutaki kutumia iPad wala Android. Tunasema hivi kwa sababu sisi katika Gajetek hatudhani kwamba Windows 7 inastahiki kutumiwa katika kompyuta aina ya tablet, hata Microsoft wanakubaliana na hilo, ndio Windows 8 iko jikoni na inatarajiwa kuiva mwishoni wa mwaka huu.
  3. Ili kuifaidi tablet hii huna budi kuwa ni mtumiaji wa simu yoyote ya Blackberry kwa sababu ya kile walichokiita Blackberry Bridge. Yaani apps kadhaa hazifanyika kazi mpaka tablet hii iunganishwe na simu kwa kutumia BB bridge. Miongoni mwa apps hizo ni pamoja na BBM.

Kuijumla ni tablet yenye kupendeza na kuvutia kimaumbile, ni nyepesi na rahisi kuibeba na inakamatika mkononi vizuri tu. Tuangalie vianisho halisi kabla ya kuendelea na uchambuzi:-


Prosesa: ina core mbili yenye kasi ya Ghz moja. Kwa sasa hii inaonekana kama ni kiwango cha kawaida kwani karibu tablet zote za hali ya juu hutumia prosesa yenye kasi hii.

RAM: GB moja, hii inaifanya tablet iwe na kasi nzuri ya kutosha. Japokuwa kwa baadhi ya wakati hutokea kuzorota, ingawa sio sana.

Kamera: Kamera ya mbele ina megapikseli 3 na ya nyuma ina megapikseli 5, zote zikiwa na uwezo wa kurekodi video za HD kamili yaani 1080p. ina poti ya HDMI kwa hiyo kuunganisha na teli (TV) ni kawaida tu.

Umbile: urefu ni 5.1″/130mm na upana 7.6″/194mm. Pia ina wembambani wa 0.4″/10mm na uzito 0.9 lbs/25g.

Skrini: Ukubwa wa skrini ni 7″ aina ya LCD rezolushani 1024 x 600, hatuna budi kukiri kuwa BB playbook inang’ara mpaka mwisho, yaani hapa haina kifani katika tablet yoyote nyingine ikiwemo iPad 2, Galaxy Tab na Motorola Zoom. BB Palybook ni tablet inayostahiki kuitwa HD ya kweli.

Sasa turudi kwenye uchambuzi, tukianza na multitasking tumesema hapo awali ni bora kuliko zote, hii ni kutokana na ukweli kwamba unapofungua multitasking apps zote zinaendelea kwa ‘live’ kwa hiyo kama unaangalia video, video hiyo inaendelea kuchezo na kama unadownload faili basi inaendelea ku-download hata ikiwa si app unayoitumia.

Vile vile tumeeleza kwamba ina nafasi ya kutoa ushindani hapo baadae, hili liko wazi kwani kikubwa kichoirudisha nyuma tablet hii ni mambo mawili:-

  1. Ukosefu wa apps za kutosha katika App World. Ni wazi kwamba apps ndio zenye kuifanya tablet iwe na matumizi mengi, mazuri na kwa mujibu wa utashi mtumiaji. Mpaka hili liweze kufikiwa Playbook itakuwa nyuma ya iPad. Hata hivyo hili si kubwa iwapo Playbook itapata mauzo mazuri basi developers watavutika kwenye kuendeleza na kuandika apps za tablet hii. 
  2. Gajetek tunahisi kwamba kuwepo kwa bridge katika kuiwezesha kushirikiana (sharing) simu za BB katika matumizi ya internet na simu ya BB ni jambo zuri, hata hivyo kuweka apps kama vile BBM, email, kalenda, contacts, memo na task kuwa ni tegemezi la simu za BB maana yake watu wote wanaotaka kutumia tablet hii hawana budi kununua simu za BB. Hili ama litawapunguzia mauzo ya tablet na/au litaongeza mauzo ya simu kwa upande mwingine.
Ukiacha udhaifu huu, Playbook ina browser iliyo maridadi na yenye kasi katika kupakia kurasa mbali mbali, ukizingatia pia kwamba inakubaliana na flash, hii inaifanya kuwa ni hoja ambayo inaipa tableti hii ubora kuliko hata iPad 2. 
Multitasking katika Playbook ni yenye ufanisi mkubwa

 Jambo jingine ambalo linaifanya tableti hii kuwa ni ya kipekee ni kule kufanya fremu yake kuwa ni sehemu ya matumizi, yaani unaweza kufungua mambo mbali mbali kwa kusugua kwenye fremu ya Playbook kwenda juu, chini, kulia na kushoto.

OS mpya ya Blackberry  Playbook inavutia mno, ina kasi ya kutosha na ni yenye kufanya kazi kwa ufanisi, mara baada ya kuitumia tumeanza kuiona mapinduzi katika gejeti za RIM, kwani tunaamini OS hii ambayo ni tofauti na ile iliyoko kwenye simu itatumika kwenye simu za baadae za Blackberry, BB OS tablet inatumia utaratibu wa QNX.

Katika sula la kuitumia kikazi, tablet hii inakuja na Apps nne muhimu Word to go, Sheet to go na Slideshow to go. Vile vile ina Adobe Reader. Mbali na hayo internet ni kwa WiFi au kupitia BB Bridge, email unaweza ama kutumia web ya kawaida au vile vile BB Bridge. Ingawa unapotumia web ya kawaida huwa hakuna ufanisi mzuri.

Kwa upande wa usalama hii haina haja ya kuzungumzia lolote kwani tunawafahamu RIM kuwa katika hili wao ni namba moja. Unaweza kuingiza mafaili kwa kutoka kwenye kompyuta kwa kutumia BB Desktop kwa sasa baada ya kuboreshwa kwa OS yake.

Sisi wa Gajetek kwa sasa tunaipa BB Playbook namba mbili baada ya iPad 2, pia ni chaguo tofauti, kwa wale ambao wangependa kuwa na tablet mbili, basi Playbook ina nafasi hiyo, pia tukumbushe kwamba 7″ inaingia kwenye mfuko wa suruali bila ya wasiwasi wowote. na kama RIM watajaribu kufanya mapinduzi ya haraka katika mwenendo wao basi tableti hii ina nafasi nzuri ya kukamata kilele hapo baadae. Kazi kwa Reseach In Motion.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s