iPhone 5 Sasa ni Septemba

 

Kizazi cha tano cha simu ya iPhone sasa kinatarajiwa kutolewa mwezi Septemba mwaka huu sambamba na iOS 5 ambayo imetangazwa wiki iliyopita katika mkutano wa WWDC wa 2011. Kwa mujibu wa wadau walio ndani ya Apple simu hiyo iko ndani ya hatua za mwisho mwisho za majaribio. Tangu kuanza uzalishaji wa simu ya iPhone mwaka 2007, kampuni ya Apple imekuwa ikiitangaza simu hiyo mwezi wa sita katika mkutano wa WWDC na kuingia madukani katika mabara ya Marekani na Ulaya mwezi wa saba. Kwa kawaida mwezi wa Septemba ni mwezi wa kutangaza iPod mpya na sio iPhone.
Mwaka huu kinyume na matarajio ya wengi na kawaida ya Apple katika mkutano wa WWDC iPhone hata haikutajwa. Ni mawazo ya wengi kwamba iPhone sasa inakaribiwa na wapinzani mbali mbali na hasa simu za HTC na Samsung. Vile vile kwa mbali kidogo Motorola na LG nao wanainyemelea simu hii. Hivyo Apple hawana budi kuiboresha zaidi simu yao, na hili limesababisha kuchelewa kwa utolewaji wa simu. 

Pia wengi wanadhani kuwa wakati umefika Apple kutoa simu zaidi ya moja badala ya utamaduni wao wa kutoa simu moja tu kwa mwaka, kwa mfano kulikuwa na matarajio mwaka huu kutakuwepo iPhone 5 pamoja na iPhone Nano. Gajetek tulipata nafasi ya kuhojiana na mmoja wa wafanyakazi wa Apple Highcross, Uingereza nae amekataa kabisa kukanusha au kuthibitisha habari hizi, hatukustaajabishwa na hili kwa vile Apple ni kampuni yanye usiri mkubwa katika bidhaa zao kabla ya uzinduzi rasmi wa bidhaa.
Baadhi ya vianisho halisi vinavyozungumziwa kuwepo kwenye simu hiyo ni pamoja na prosesa ya A5 iliyotumika kwenye iPad 2, prosesa hii ina core mbili na kasi ya Ghz moja, kwa madai ya Apple vile vile ina matumizi madogo sana ya betri, hili linathibitika kwa bidhaa ya iPad 2 kuwa na betri yenye kutumika masaa tisa, iwapo utaichaji iPad 2 kwa mpaka 100% bila ya kuitumia betri inadumu mwezi mzima. Vile vile kamera ya simu hiyo inatarajiwa kuboreshwa na kuwa na megapikseli nane pamoja na HD kamili yaani 1080p. Hata hivyo haya yote si mageni tayari katika soko kuna simu kama vile HTC Evo 3D ambayo ina vianisho bora zaidi kuliko tunavyotarajia kuwemo katika iPhone ijayo na Evo 3D imwshatangazwa rasmi na HTC na itatolewa mwishoni mwa mwezi huu.
Tunaamini kwamba mbali na matarajio pamoja na uvumi wa vipi itakuwa iPhone ijayo, Apple hawataacha kutushangaza kwa kuingiza mamba ambayo hakuna aliyetarajia. Hii ni kawaida kabisa, prosesa ya A4 na kioo cha retina katika iPhone 4 havikutarajiwa, iPad ilipokaribia kutoka wengi walidhani kuwa itatumia Mac OS X lakini badala yake ikatoka na iOS na pia iBooks iliwavutia wengi, iPad 2 haikutarajiwa kutoka na smart cover na mengine mengi, Je, Apple watatushangaza na nini katika iPhone 5? Septemba haiko mbali na tunaamini kuna jambo ambalo litakuwemo kwenye simu hiyo ambalo halipo kwenye simu yoyote nyingine.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s