ForceShoe: Viatu teknolojia tupu.

 

Kampuni ya Xsens wamenunua haki miliki ya viatu vilivyopewa jina la ForceShoe kutoka Chuo Kikuu cha Twente kilichopo Uholanzi, lengo la ununuzi huo ni kufanya utafiti zaidi juu ya viatu hivyo, hivyo XSens watakuwa tayari kuwapa watafiti mbali mbali wa fani ya Biomechanic ili kuviendeleza viatu hivi zaidi.

Forceshoe vina uwezo wa kutoa takwimu za mwendo wa mvaaji ambazo zitasaidia kujua udhaifu wa sehemu mbali mbali za mwili unaopelekea kuwa na matatizo katika mwendo. Miongoni mwa walengwa wa viatu hivi ni pamoja na wagonjwa ambao wanaanza mazoezi ya kutembea kutokana na athari walizozipata zilizopelekea kushindwa kutembea, pia viatu hivi vinaweza kutumika na wanamichezo mbali mbali na hasa wale wanaotumia miguu zaidi katika michezo yao. Kundi jingine litakalotumia viatu hivi ni wanasayansi wenye kufanya uchambuzi wa mwendo na namna misuli inavyofanya kazi katika mwili wa binadamu (Gait analysis).
Miongoni mwa vijimambo vilivyowekwa kwenye viatu hivi ni sensa aina ya MTx zenye kuweza ‘kuhisi’ na kutoa taarifa za mwendo, transceiver ya bluetooth yenye USB, Xbus Master ambacho ni kifaa chenye uwezo kudhibiti mwendo baada ya kupokea taarifa za mwendo, kwa maana hii viatu hivi vitamrahisishia mtembeaji kazi ya kutembea na kumsahihisha pale anapokosea. Vile vile viatu hivi vinauwezo wa kupeleka taarifa mbali mbali kwenye kompyuta bila ya kutumia waya, taarifa ambazo zitatumika na wataalam kujua matatizo aliyonayo mtembeaji na maendeleo na mabadiliko yanayotokea kwa mtembeaji kila anapovitumia viatu hivi.
ForceShoe kwa sasa havitegemewi kuanza kuuzwa mpaka pale utafiti utakapokamilika juu ya namna ambavyo vinaweza kumsaidia mwanadamu katika maisha yake. Viatu hivi vinaweza kuvaliwa mahala popote bila ya masharti yoyote.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s