Blackberry OS 7 kutumia QNX?

Bold 9900 kutolewa karibuni

Research in Motion maarufu zaidi RIM watengenezaji wa simu na tableti za Blackberry huenda wakatumia platfomu ya QNX katika toleo lijalo la OS ya simu zao. Hili linaonekana kuwa na uwezekano mkubwa kwa vile RIM wametumia platfomu hiyo katika tablet yao yaani Blackberry Playbook. Playbook imeshaingia madukani huko Marekani na inategemea kutolewa ulaya kuanzia tarehe 15/06/2010.

QNX inafanya kazi tofauti kabisa na Blackberry OS 6 inavyofanya kazi, QNX ni kifupi cha Quick UNIX, kikubwa platfomu hii hutofautiana na OS nyingine zote za simu na tablet kwa kuendesha operesheni zake kwa kutumia servers, servers kwa maana ya ‘vijitask’ vidogo vidogo (Si server ya mtandao) ampabo OS nyingine za simu na tablet hutumia kile kinachojulikana kama monolithic kernel model ambazo ni operesheni kubwa ukilinganisha na zile za QNX. Hii huipa nafasi OS inayotumia QNX kufanya kazi pevu kwa kutumia nguvu kidogo.

Vile vile kwa upande wa developers wanaweza kuzima baadhi ya servers zilizoko kwenye OS ambazo hazitumiki katika apps zao na hivyo kuiwezesha app kuwa na ufanisi na kasi zaidi. Mpaka hapo inatosha kupata picha kwamba OS iliyotumika kwenye Blackberry playbook ina nafasi ya kuwa OS iliyo na ufanisi na kasi zaidi kuliko OS zote zilizoko kwenye soko kwa sasa ikiwa ni pamoja na iOS ya Apple. Kumbuka tumesema kuwa ina nafasi, hii itategemea zaidi ni vipi wataalam wa RIM wataweza kuiendeleza OS hii.
OS ya Playbook inatumia QNX
Hata hivyo kwa namna ilivyo Blackberry OS ya Playbook ambayo tayari ina ufanisi mzuri katika mambo mbali mbali na hasa namna multitasking inavyofanaya kazi, ni wazi kwamba RIM wamepakia kazi zinazohitaji kifaa chenye kasi, kwa wastani ni lazima simu ambayo itatumia Blackberry OS tablet iwe na prosesa ya Dual core. Tunaweka msisitizo hapa kwamba si matumizi ya QNX yanayohitaji prosesa yenye nguvu bali namna RIM walivyoweka mambo mengi yenye kuhitaji prosesa yenye nguvu kwenye OS yao.
Sasa ikiwa ni kweli kwamba RIM wataleta OS hii kwenye simu za Blackberry maana yake ni nini? Hapa ndipo tunapotaka kuingia kama wachambuzi wa Gajetek. Faida ni nyingi, baadhi yake ni:-
  • Kwa mara ya kwanza tutaiona Blackberry yenye vianisho halisi vya hali ya juu, na hivyo simu yenye nguvu kwa prosesa, RAM na hivi vitaendana na skrini yenye mng’aro wa wenye kuvutia.
  • Tutaweza kuwa na simu yenye utendaji (impelementation) wa multitasking bora kuliko simu zote zikiwezo za iOS na Android.
  • Tutaweza kuwa na simu yenye ufanisi wa hali ya juu katika nyanja zote kwa vile QNX ni rahisi kuitumia na kama tulivyoeleza ina kasi nzuri.
  • Kwa vile developers wataweza kuzima baadhi ya servers ni wazi kuwa apps nyingi zitakuwa na kasi nzuri katika simu hizi.
  • Huenda ikavutia developers wengi na hivyo Blackberry AppWorld kutoa ushindani wa kweli kwa App Store ya iOS na Android Market ya Google vile vile Windows Marketplace ya Microsoft.
  • Watumiaji wa Blackberry watahisi mabadiliko makubwa yenye manufaa mengi kimatumizi na hata kwa apps, mambo ya game kama vile FIFA na Need For Speed yatakuwa ni yenye kupendeza kwenye platfomu hii.
Lakini pia kwa wale wanaotumia Blakcberry zilizopo sasa, hakuna ambayo itaweza kutumia Blackberry OS 7 ikiwa itatengenezwa hivi, hivyo basi kutakuwa hakuna uboreshwaji (upgrade) kwenye simu zao.
Kwa upande wa RIM, faida pia ni nyingi:-
  • Wataondokana na kuitegemea Blackberry Messenger na ufanisi katika usalama (encryption) kuwa ndio vivutio pekee katika mauzo, kwani wataweza kutoa ushindani wa mzuri katika soko la simu.
  • Watajitendenezea soko kubwa, kwani hata wenye Blackberry tayari watataka kununua Blackberry mpya kutokana na ubora utakao kuwepo na tofauti kubwa.
Mwisho kabisa labda tuseme, umefika wakati RIM hawana nafasi tena ya kuzembea kwa vile kama suala ni BBM tayari kuna iMessage kwenye iPhone, iPad na iPod Touch. Windows wameshanunua Skype na inasemekana Google wako jikoni nao na si muda mrefu watatoa app yao ambayo imeambatanisha na Andriod ka ajili ya kuchati. Lazaridis Afisa Mtenda Mkuu Mwenza wa RIM analifahamu hili, RIM mnasubiri nini?
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s