Wii U Yavutia Hisia za Wengi

 

Wakati mkutano wa waandika apps wa Apple WWDC ukiendelea San Fransisco, huko Los Angeles Convention Center maonyesho wa michezo ya kompyuta E3 nayo yanaendelea, baada ya Sony na Microsoft kuonesha yao, Nintendo ndio walioshusha gajeti iliyoteka hisia za wahudhuriaji wengi, gajeti hiyo ni kizazi kijacho cha Nintendo Wii ambacho kitaitwa Wii U. Wakielezea kuhusu dhana ya jina hilo Nintendo walisema Wii inaashiria We ya sisi na U inaashiria You yaani wewe, kwa hiyo Nintendo  wanamaanisha kwamba hii itakuwa ni konsoli yetu, yaani tuzeche sote lakini ni konsoli binafsi pia yaani itakufurahisha wewe. Ni lugha ambayo ina falsafa kubwa ndani yake.

Tuanze na badiliko kubwa kabisa katika konsoli hii nalo ni kontrola za aina yake. Nintendo wameshusha kontrola yenye skrini kubwa kuliko skrini ya PSP (PS Vita), ikiwa na ukubwa wa inchi 6.2, kontrola hii yenyewe inaonekana kama ni konsoli ya mkononi mfano wa PS Vita au DS Lite, lakini Nintendo wametahadharisha kuwa hiyo ni kontrola na haiwezi kufanya kazi peke yake. Hata hivyo kontrola hii ina mengi kwanza tuelezee konsoli yenyewe na kontrola tutaiandalia maada yake.
Wii U inakuja na HD kamili, yaani 1080p hapa Nintendo wamechelewa mno kwani Wii ya sasa ina standard definition. Lakini tuseme wazi kuwa hapa wamelenga kuingia kwenye mkumbo wa uhalisia hali ya kuwa wanajua wazi kuwa hichi si cha kuvutia mauzo tena. Jambo jingine muhimu kuhusu Wii U ni kwamba kontrola za zamani na vikorokoro vyote vya Wii vitaendelea kufanya kazi na Wii U.

Konsoli hii pia itakuwa na flash memory. Nintendo hawakueleza wazi juu ya kiwango cha ukubwa wa memory yake. Ukiondoa disk ya ndani Wii U pia itakuwa na uwezo wa kupakia kadi ya SD na uwezo wa kuchukua disk za nje (USB HDD). Kwa vile Wii U imeingia katika uwanja wa HD, DVD zao mpya zitakuwa zina ukubwa wa GB 25, ingawa pia Nintendo wamewahakikishia wapenzi wa konsoli hiyo kwamba itaendelea kuwa na uwezo wa kusoma disk za zamani. Konsoli hii pia itakuwa na kamera itakayo waruhusu wanaocheza kupitia mtandao kufanya video chat.

La kusikitisha ni moja tu, tutakuwa na muda mrefu wa kuisubiri konsoli hii, Nintendo wamekataa kutaja tarehe ya kutolewa, lakini wameahidi itakuwa ni mwaka 2012, tunakukumbusha kuwa usisahau kuchungulia chungilia kwenye Gajetek kwani kwenye makala zijazo Mungu akipenda, tutajadili na kuchambua kivutio kikubwa cha konsoliya Wii U ambacho ni kontrola mpya yenye skrini.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s