Wii U na Kontrola ya Kipekee

 

Kwanza kabisa turudi nyuma miaka kadhaa, ilipotoka PS3 na XBox 360, HD ilikuwa ndio kivutio kikubwa cha mauzo, wakati PS3 ilitoka na blue Ray, XBox 360 ilitoka na HD. Nintendo walipotangaza kwamba Wii itakuwa na Standard Definition wengi wakadhani kwamba wameshapigwa bao na wamekwisha. Wii ilipotoka walikuwa na kivutio kimoja, nacho ni Wiimote, kontrola ya kwanza kuwa na sensa ya mtikisiko (Motion Censor), muda mchache baada ya mchezo kuanza Nintendo Wii ikawa inaongoza kwa mauzo na kuwapita wapinzani wake kwa kiwango kikubwa, ikabidi PS3 watengeneze kontrola kama hiyo na XBox wakaja na Kinect kifaa ambacho kinaufanya mwili wako kuwa ni kontrola. Bila ya shaka kontrola ni ‘big dil’ katika konsoli.

Wii sasa inaonekana haina mpya yoyote, kumbe Nintendo wako jikoni, sasa chakula kinaribia kuiva, wametangaza na kuonesha kwenye maonyeshoya E3 konsoli yao mpya, nayo ni Wii U. Kwa mara nyingine kivutio kikubwa katika konsoli hiyo ni Kontrola. Tofauti wa WiiMote kontrola hii bado haijapewa jina lakini tuna uhakika kwamba wataalam wa Sony na Microsoft vichwa vinawawasha kufikiria namna ya kukabiliana nayo katika ushindani wa kibiashara, mimi nadhani itawabidi  wakubali kuwa ni ‘copy cats’ yaani baadae kidogo hili wataliiga tu, hawatakuwa na ujanja. 
Tukianza na kivutio kikubwa kabisa ambacho hakuna aliyekitarajia Nintendo wameweka kwenye kontrola hiyo skrini yenye ukubwa wa inchi 6.2, labda tuwakumbushe machache kuhusu ukubwa huu. Sony PSP Skrini yake ni inchi 5, book reader ya Amazon, yaani Kindle 2 ina ukubwa wa inchi 6 na HTC Flyer ina ukubwa wa inchi 7. Kwa hiyo tunaona ni jinsi gani skrini hii livyijimiksi vizuri mchezoni.
Skrini hii inatumika kwa namna ya kipekee, utakapoishusha chini itakuwa ni kontrola tu, utakapoinyanyua juu na kuiweka sambamba na uso, game inahama kutoka kwenye skrini ya TV kuja kwenye skrini ya kontrola, kwa hiyo unaweza kucheza game bila ya kutumia TV kabisa ikawa ni kama konsoli ya mkononi (portable console), tayari wengi wameanza kujiuliza niisubiri Wii U au niendelee na mpango wangu wa mwanzo wa kununua PS Vita? Ni swali gumu ikiwa Wii U utashuka na mambo kama haya. Yaani mshikaji kainigia anakuzingua oo kuna habari muhimu kwenye Telly weka CNN, wewe unamuacha na CNN yake wewe unakula game kwenye skrini ya kontrola, habari baadae. Mambo ndio hivyo.
Yaani kuna mengi ya kuchambua kuhusu kontrola kuliko konsoli yenyewe, kontrola hii pia ina kamera ambayo unaweza kuwa na video chat unapocheza game na mpinzani aliyekuwa kwenye mtandao (online gaming), ukishamfunga sana huenda ukimuona alivyosawajika ukamuonea huruma, ukamuachia kidogo kumpunguzia huzuni, mpinzani huyo akileta jeuri unamtwanga tena.
Kontrola hiyo ina joystick mbili kulia na kushoto, ina sensa ya gyroscope na accelerometer zitakazosaidia kujua kwamba unatumia skrini ya TV au unataka kutumia skrini ya kontrola, hakuna haja ya kubinya swichi yoyote ile, ni wenyewe tu inajibadilisha, yaani miaka michache iliyopita tungejiuliza jamani huu ni uchawi au vipi? 

Vile vile ina kifungo chenye umbile la alama ya kujumlisha kama kile kilichopo kwenye Nintendo 3DS au DS Lite. Cha kufurahisha zaidi ni kwamba skrini ya kontrola hii ni skrini ya kugusa (touch screen) na itakuja na kijiti chake (Stylus) ingawa pia utaweza kutumia vidole. Ina kijimaykrofoni cha kuchukulia sauti kwa ajili ya kuchati kwa sauti tu au video.
Kwa kifupi washabiki wa Nintendo tayari wameshapagawa na kontrola hii ambayo inatubidi tuisubiri mwaka mzima, ama kweli hajakosea aliyesema ngoja ngoja inaumiza matumbo, washabiki wa Nintendo watakuwa taabani, hii ni kutokana na ukweli kwamba Wii U itatoka mwaka 2012. 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s