Playstation Vita Sasa ni Jina Rasmi

 

Wiki iliyopita tuliwadokezeeni habari za kuvuja kwa jina halisi la NGP, kizazi kijacho cha PSP kuwa itaitwa PS Vita, Jana katika maonyesho ya Electronic Entertainment Expo (E3), Sony imethibitisha na kulitangaza rasmi jina hilo. Pamoja na  jina, Sony pia imetangaza bei za Marekani na Ulaya za gajeti hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa.

Ikitangaza bei, Sony wamesema PS Vita yenye WiFi pekee nchini Marekani itauzwa $249.00 na Ulaya itauzwa €249.00, na ile yenye 3G na WiFi itauzwa Marekani kwa $299.00 na Ulaya itauzwa €299.00. Kwa mtindo huu ambapo inaonekana Sony inabadili aina ya sarafu tu lakini bei ni ile ile, basi huenda kama Sony wangeuza gajeti hii Tanzania ingekuwa TSh 249.00 na TSh 300.00, lakini kwa bahati mbaya Sony huwa haiuzi bidhaa zake Bongo moja kwa moja. Wabongo tungechekelea na kufungua maduka yetu ya bidhaa za Sony Ulaya na Marekani na kuwarudishia kwa bei poa bila hasara. Huenda Sony wameliapuka hili. 
Tukiachana na utani, Sony pia wametangaza baadhi ya game ambazo ziko tayari kwa PS Vita, miongoni mwa game hizo ni pamoja na Street Fighter x Taken,  ModNation Racers na LittleBigPlanet. Game zinazopendwa na Waswahili bado hazikuonekana. Hata hivyo tusiwe na wasi wasi kwani kuanzia sasa hadi Disemba itakapotoka Playsatation hii bado muda ni mrefu. Halafu konsoli bila ya FIFA na PES basi bado haijawa Konsoli.  


Kwa vile jina hili ni jipya basi tungependa kuwatahadharisha Waswahili wenzetu kwamba tusije kuiita konsoli hii ‘pii es vita’ Sony wenye wakitusikia watazua vita, bali hutamkwa ‘pii es vayta’.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s