iCloud kuingia kwa namna yake.

 

Cloud si jambo geni, lina maana ya huduma ya kuweka mafaili, program na mambo mbali mbali kwenye mtandao badala ya kuhifadhi kwenye disk ya kompyuta, kwa maana hii wengi wameitangulia Apple kwenye huduma hii, lakini Apple wamekuja na mtindo wa pekee ikiwa ni sehemu ya pili ya huduma ya cloud kutolewa na kampuni hiyo baada na badala ya MobileMe. Afisa Mtendaji Mkuu wa Apple, Steve Jobs, katika hali ambayo sio ya kawaida amekiri kwamba Apple wamechemsha katika huduma ya MobileMe.

Kwa watumiaji wa MobileMe, huduma ambayo inafutw iClouds itakapoanza, huenda wakawa na mchanganyiko wa furaha na huzuni. Tukianza na lenye kuhuzunisha, watumiaji wa iCloud watakuwa na uwezo wa kuhifadhi mafaili mwisho 5GB, wakati kiwango cha chini kabisa kwa wenye kutumia huduma ya Mobile Me ni 20GB na unaweza kuongeza 20GB nyingine na kuwa na 40GB au hata zaidi.
Sasa tuingie kwenye yenye kufurahisha kwa watumiaji wa zamani wa MobileMe na watumiaji wapya watakaojiunga na iCloud,  Huduma hii itakuwa ni bure na tena imeboreshwa, ubora wa hali ya juu. Kwa mujibu wa Apple huduma hii itahifadhi muziki, picha, apps, kalenda, dokumenti na mengine mengi kwenye mtandao bila ya kuunganisha kwa waya vifaa mbali mbali unavyovimiliki. Mafaili yatakuwa yanaji-sync wenyewe baina ya vifaa vya iOS na kompyuta. Gajeti zinazojumuishwa katika huduma hii mpya ni pamoja na kompyuta zikiwemo za Windows, iPad, iPod Touch na iPhone. Huduma hii itaanza rasmi baada ya kumalizika kwa msimu wa kiangazi cha Ulaya mwaka huu, kwa hiyo ni kwenye mwezi wa Septemba hivi. 
Kwenye gajeti za iOS (iPod, iPhone na iPad) watakuwa na apps tisa ambazo zinatumia huduma hii. Apps hizo ni Contacts, Calender, Email, App Store, iBooks, iPhoto na iTunes. Vile vile kutakuwa na Apps mbili mpya kabisa kwenye vifaa vya  iOS nazo ni iCloud na Documents. 
Tukianza na ITunes;  utakaponunua au ku-download chochote kwenye kifaa chako kimoja, kwa mfano Iphone, iphone yenyewe itapeleka mafaili haya kwenye iCloud na iCloud itarudisha kilichonunuliwa kwenye kompyuta, iPad na ipod Touch unazomiliki, sharti ni kwamba zote ziwe zinatumia akaunti ya iTunes moja. iMessage nayo itakuwa inafanya hivyo hivyo baina ya vifaa vyako vya iOS. tukienda kwenye iBooks, kitabu chochote utakacho download wenyewe kitapelekwa kwenye vifaa vako vyote, vile vile utakaposoma kitabu kwenye iPhone na kuweka alama ya ilpofikia (bookmark) alama ile itapelekwa kwenye vifaa vyako vyote. 
iCloud itasaidia sana kuondoa wasi wasi wa kupoteza mafaili iwapo kifaa chako kitapotea au kuharibika kwa namna yoyote. Kwa  upande wa iPhoto vifaa vya iOS vitahifadhi picha 1000 za mwisho, kompyuta itakuwa haina kiwango maalum, yaani itahifadhi picha zote.
Apps zitakazotumia iClouds
iCloud imeondoa kabisa suala la ku-sync iPod au iPhone na iPad kwenye kompyuta yako kwani  vile vile itakuwa inafanya backup ya vifaa vyako kwa kusaidiana na kile ambacho Apple wamekiita ‘PC Free’ ambayo tutailezea tutakapozungumzia iOS 5, na kurudisha Kompyuka kihadhi kuwa sawa na simu na tablet katika kutegemeana.  
Japokuwa Apple wamesema kwamba iClouds ni bure lakini sharti lake ni kuwa bure hiyo ni kwa wale wanaomiliki vifaa vya iOS, kama unatumia Blackberry, Motorola, HTC na gajet za kampuni nyingine basi kwenye bure hii humo. Kwa hiyo Apple wanalenga kuvuta wateja zaidi kwa kutumia huduma hii. 
Vile vile watumiaji wa Apple TV wataweza kutumia iClouds na kufaidika na vile vilivyomo kwenye gajet zao zote. Kwa wale wenye email za MobileMe yaani jinalako@me.com wasiwe na wasi wasi wowote kwani Apple itahamisha email yako moja kwa moja kwenye huduma ya iClouds. Septemba haiko mbali tukiwa na uhai, Gajetek tunaisubiri kwa hamu iClouds iingine uwanjani.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s