HTC Evo 3D: Ni mwisho wa Njia

Weka pembeni Salsa na Chacha simu ambazo HTC wamezitoa zikiwa na kivutio cha mauzo kimoja tu, nacho ni Facebook. HTC wamerudi tena ulingoni na kutwanga ngumi moja ya nokaut (knock out), Ngumi hiyo ni HTC Evo 3D. Yaani mambo yako hivi, Umenunua TV yenye uwezo wa 3D lakini unajihisi kuwa hakuna programu za kutosha za 3D hivyo unapunjika, sasa tulia kwani unaweza kufungua studio yako ya 3D kwa simu hii. Kamera yake ina uwezo wa kurekodi na kupiga picha katika kiwango cha 3D, lakini kinachofurahisha zaidi ni uwezo wa skrini ya simu hii kuonesha picha na video za 3D bila ya kutumia zile miwani nzito zenye kuchosha.

Vianisho halisi vya HTC Evo 3D ni kama ifuatavyo:
CPU: 1.2 GHz dual-core prosesa, ni aina ya Adreno 220 GPU, Qualcomm MSM8660. Kwa sasa hii itakuwa simu yenye CPU yenye nguvu kuliko simu zote. 
Kamera: Ina megapikseli 5 MP, yenye kutoa picha zenye pikseli 2560х1920, ina autofocus na dual-LED flash. Ina stereoscopic photos (2 MP tu); pia ina uwezo wa kufanya ‘geo-tagging’ yaani inaweka kumbukumbu za kijiografia juu ya mahali ambapo picha imepigwa. Video ndio noma, 1080p@24fps (2D), 720p@30fps (3D). Kamera ya mbele ina megapikseli 1.3 tu.
Skrini: Ina ukubwa wa inchi 4.3 yenye 3D S-LCD capacitive ya kugusa, teknolijia hii ndio yenye kuipa uwezo simu hii wa kuonyesha 3D bila ya miwani. Kiwango cha rangi ni 16 milioni pia ina pikseli 540 x 960. Skrini yake vile vile ina accelerometer, yenye kuiwezesha kugeuza unachotizama kwenye skrini unapoigeuza simu, pia ina sensa za proximity na gyro. Simu hii imevalishwa koti la HTC Sense kama user interface, lenye kubadili skrini kwa manjonjo ya 3D. 
RAM na Kuhifadhi mafaili: Simu hii ina gigabayti nzima ya RAM na pia ina unawezo wa kupakia kadi aina ya micro SD yenye ukubwa mpaka gigabayti 32. Bado tunasubiri simu itayayoingia gigabayti 64, ingawa 32 sio mbaya kwa sasa, lakini ukizingatia kwamba simu hii inarekodi 3D movie nadhani HTC walikuwa wasogee mbele kidogo katika suala hili.
Mpaka hapa inatosha simu hii kuiondoa Samsung Galaxy S2 kwenye kilele cha simu kumi bora itakapotolewa. Kuhusu ukubwa ina vipimo 126 x 65 x 12.1 mm, hivyo si simu iliyelengwa kuwa nyembamba sana. Hata hivyo upana wa milimita 12.1 si wa kuchukiza inapoikamata mkononi. Simu hii inakuja na huduma mpya inayojulikana kama HTC watch ambayo unaweza kuangalia ‘Hollywood Movies’ kwenye simu yako.  OS yake ni Android 2.3 Gingerbread.
Kikubwa chengine kama tulivyoeleza hapo juu ni kwamba unaweza kuunganisha na TV yako kwa kutumia HDMI na hivyo kuangalia movie zako za 3D kwenye skrini kubwa. Nadhani karibu utafikia wakati tutajiuliza ni kwa nini ninunue kamkoda, kamera na DVD wakati nina simu. Huko nchini Marekani simu hii itaingia madukani tarehe 24 mwezi Juni mwaka huu. Tunaisubiri kwa hamu kuona kama 3D ina ubora uliokamilika. Tazama video hapo chini mwenyewe upate uhalisia kiasi fulani juu ya simu hii

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s