Wateja wa Apple Wavunjika Moyo

>

Steve Jobs kwenye keynote ya WWDC 2011, mjini San Fransisco
Wengi walikuwa wakisubiri kwa hamu mkutano wa World Wide Developers Conference 2011 unaoendelea huko San Fransisco, Marekani wakiwa na matarajio kwamba Apple watatangaza iPhone 5. Hata hivyo baada keynote ya masaa mawili kumalizika walivunjika moyo kuona kwamba iPhone 5 haikutangazwa.
Pamoja na kukosekana kwa iPhone 5 mkutano huo uliripuka na kushangilia kwa vifijo na makofi mara kwa mara kwa vivutio mbali mbali vilivyokuwepo. Kivutio cha mwanzo kabisa ni pale Afisa Mtendaji Mkuu wa Apple, Steve Jobs alipoibuka ukumbini na kufanya ufunguzi, ilimchukua muda kidogo akisubiri developers waliomlaki kwa makofi na mayowe ya kushangilia wanyamaze ili awakaribishe na kufanya ufunguzi rasmi. Baadhi ya watu walikuwa na wasi wasi huenda Jobs asingekuwepo kutokana na kusambuliwa na ugonjwa wa saratani (kansa) ya Pancreas. Hata hivyo Steve Jobs alionekana wazi kuwa amedhoofika kiafya.


Mbali na hilo kivutio kikubwa zaidi ni kutangazwa kwa huduma ya iCloud ambayo imemaanisha kwamba huduma ya MobileMe ndiyo inaingia kaburini. Vile vile kama ilivyokuwa  matarajio ya wengi Apple wametangaza iOS 5 kwa ajili ya iPhone, iPad na iPod Touch. Pia Mac OS Lion inayotumika kwenye kompyuta za Mac iitangazwa. Zote ziliwavutia wengi zilipokuwa zikielezewa na Apple wameahidi kuanza mauzo ya Lion mwezi ujao na iOS 5 baada ya kumalizika kwa kiangazi. Hii imetowa fununu kwamba ule uvumi kuhusu iPhone 5 kuwa itatolewa mwezi wa Septemba ulikuwa sahihi.
Mkutano huo umehudhuriwa na watengeneza Apps na waandishi 5,200 kutoka nchi 120 Duniani. Kulikuwepo pia wataalam 1000 wa Apple pamoja na maabara 100, ambapo wataalamu hao waliwaonyesha wahudhuriaji namna OS hizi pamoja na clouds zinavyofanya kazi na kuwaelimisha ni vipi wanaweza kutengeneza Apps zao ziendane na OS mpya hizo. Mkutano wa  WWDC 2011 utaendelea kwa muda wa siku tano.
Stay tuned, kwenye makala zijazo tutaelezea kinagaubaga kuhusu operating system hizo pamoja na huduma mpya ya iCloud, Mungu akipenda. Baaada ya mkutano huu je ni wapi Apple wanaelekea? Yote haya tutayajadili. Hii ni wiki ya Apple katika blogi ya Gajetek.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s