Siri ya Mafanikio ya Apple

Steve Jobs kwenye WWDC 2011
Mkutano wa WWDC 2011 leo unaingia siku ya pili kati ya tano, jana katika mkutano huu Apple wamedokeza baadhi tu ya mfanikio ambayo kampuni hiyo imeyapata. Takwimu mbali mbali zimetolewa ambazo zinaashiria kwamba Apple wanaelekea kwenye ukiritimba katika mauzo  ya bidhaa mbali mbali. Ikiziona baadhi ya takwimu utashaangaa na kujiuliza sasa kampuni zinazoonekana kubwa kama vile Google, RIM (Watengenezaji wa Blackberry) na Microsoft ziko wapi na zinaelekea wapi.

Tupitie baadhi tu ya takwimu ili kupata picha halisi. Mauzo ya bidhaa zinazotumia iOS yamekwisha pindukia milioni 200. Ikiwa ni miezi kumi na nne tu tangu iPad kutolewa Apple wamekwisha uza  iPad 25,000,000. iTunes Store imeuza nyimbo 15,000,000,000. Duka la iBook ambalo nalo lina miezi 14 tu limeuza vitabu (E Books) milioni 130.
Appstore tayari ina apps laki nne na robo, na mpaka sasa Apple imeshawalipa developers Bilioni mbili na nusu. Apple ina maduka matatu makubwa ukiondoa yale maduka ya mitaani nayo ni App Store, iBook Store na iTunes, waliojisajili kama wanunuzi katika maduka haya ni watu milioni 225. 
Sasa takwimu hizi maana yake ni nini? Hili ndio hasa tunataka kulizungumzia. Mafanikio haya hayakuja kirahisi. Yametokana na mchanganyiko wa sababu mbali mbali. Baadhi ya sababu hizo ni ubunifu wa hali ya juu katika bidhaa zao ambazo nyingi kati ya hizo zinatamba katika soko. Tutoe mfano, kwa sasa ni wachache watapinga kwamba iPad 2 ndio tablet nzuri kuliko zote, iPhone 4 ilikuwa katika kilele cha simu bora katika chati zinazoandaliwa na wanagajet mbali mbali kwa muda mrefu. iPod zimesababishwa jina la Walkman kusahauliwa na sasa karibu sasa tutasahau MP3 player kwa ukiritimba wa iPod katika soko hili. Sasa hivi mauzo ya Kompyuta za Mac yameongoza mauzo ya kompyuta zote kwa muda wa miaka mitano mfululizo. 
Kwa hiyo ni wazi sababu kuu ni ubora wa bidhaa. Sababu ya pili ni ushirikiano mzuri na developers. Apple imekuwa ni kampuni ya kwanza kutoa asilimia 70% ya mauzo ya Apps. Hii iliwavutia developers wengi na ndio maana sasa App Store ina apps 425,000. Hii imewafanya developes hawa wajihisi kuwa ni familia katika Apple. 
Mbali na ushirikishwaji wa waandishi wa Apps pia Apple wamefanikiwa kuvutia wengi katika upande wa software kwa kuweka bei ya chini mno kwa apps zao ikiwa ni pamoja na operating system.  Kwa mfano OS yao mpya Mac OS Lion itauzwa $29.00 ambapo Windows 7 inauzwa zaidi ya $200.00 kwa key moja tu. Tusisahau kuwa ukinunua Mac OS Lion unaweza kuinstall kwenye kompyuta zako zote. Hata ukiwa na kompyuta kumi.
Kushusha bei na hivyo kuondosha ushindani katika bidhaa ambazo Apple wanaelekea kupata upinzani ni mtindo ambao sio mzuri lakini umewasaida sana Apple. Kwa mfano iPad 2 pamoja na ubora wake imeuzwa kuanzia $ 400.00 Samsung Galaxy Tab 10.1 ilikuwa iuzwe $800.00 hata hivyo baada ya kutangazwa kwa iPad 2 Samsung walilazimika kushusha bei ya Galaxy tab, wengi wangependa kuuza tablet za kiwango cha juu lakini wanajikuta wakikwama kutokana na hili. Tukumbuke kwamba Apple ni kampuni kubwa hivyo ina uwezo wa kununua malighafi ya bidhaa zao kwa bei ya chini kwa vile wananunua kwa wingi mno.
Mtindo wa kibiashara wa Apple pia unachangia kuwapa mafanikio haya, Apple hulenga kupata faida kwenye bidhaa ambazo hazina ushindani mkubwa hasa kompyuta za Mac na iPods. iPad na iPhone bado zinaelekea kupata upinzani wa karibu hivyo basi utakuta Mac na iPad zinauzwa bei ya juu wakati iPhone na iPad haziko mbali na bei za washindani ua hata huuzwa rahisi kuliko bidhaa za wapinzani wao, kwa mfano iPad 2 ya 32 GB nchini Uingereza inauzwa £ 479.00 na 579.00 wakati HTC Flyer inauzwa £600.00 ambayo nayo ina 32GB, ni wazi kuwa Flyer imezidiwa kila kitu na iPad 2. Wakati wanawaumiza washidani katika bidhaa hizi wao pia wanendelea kupata faida kubwa kwenye bidhaa zisizo na ushindani. Nukta hii inaonekana kufanana na nukta ilyopita lakini zinatofautiana kwamba ya juu ni kuwaumiza washindani na hii ni kuhakikishia malengo ya muda mrefu ni kufanya ukiritimba hata ikibidi kwa sasa wasipate faida kubwa.
Pamoja na yote haya Apple bado wanafanya kampeni kubwa za kuzitangaza biashara zao. Hivi karibuni Apple imeipiku Google kuwa ni jina (brand) namba moja Duniani, sehemu ya mafanikio haya ni uzuri wa bidhaa zao lakini sehemu nyingine ni matangazo yao.
Kuwawahi wapinzani na kuwafanya wapinzani wao ni wenye kuangalia Apple wanafanya nini. Kwa mfano simu za aina ya candy bar (mfano wa iPhone) zimepata umaarufu baada ya kutoka kwa iPhone ya kwanza. Mwaka 2011 katika teknolojia unaitwa ni mwaka wa utitiri wa tablet, hii ni kutokana na mafanikio ya iPad mwaka jana. Kwa kifupi hakuna kampuni ambayo imeweza kuwatangulia Apple kutoa bidhaa mpya na kukubalika na wateja kama Apple, kwa hiyo wote wamebaki kuwa “copy cats”
Siri nyingine kubwa ni maduka yao wenyewe. Maduka haya mbali na kuwa ni sehemu ya kuuza bidhaa pia yamekuwa ni sehemu za kuwaelimisha wateja bila ya kuwatoza fedha. Apple huendesha semina kila wiki katika maduka yao kuhusu bidhaa zao, hii imewawezesha kujenga mahusiano mazuri na wateja. Pia imekuwa ni rahisi kuwashughuikia wateja baada ya kuwauzia bidhaa. Kwa mfano simu ya HTC inapoharibika wakati bado ina waranti, inakubidi uirudishe na kusubiri zaidi ya wiki mbili ili utengenezewe simu yako. Lakini iPhone inapoharibika unakwenda duka la Apple na kuwaachia iPhone yako na hapo hapo unapewa iPhone nyingine. Kwa hiyo maduka haya unapiangalia financial statements za Apple si yenye kujiendesha kwa faida. Huwa yanapata hasara ambayo hufunikwa na mauzo makubwa ya kampuni hiyo lakini Apple wanaendelea kufungua maduka mapya kwani kwao maduka haya ni sehemu ya matangazo na huduma bora kwa wateja.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s