Simba Anguruma Kwenye WWDC

Ni Mac OS Lion, Apple wamerudi uwanjani na makeke, safari hii wameamua kuimarisha OS zao, yaani Mac OS X ya kompyuta na iOS ya iPad, iPhone na iPod touch. Vile vile wameamua kuja na huduma mpya ya iCloud ambayo ni huduma ya wakati tulio nao mbele. Tukianza na uchambuzi wetu tutaangalia juu ya Mac OS Lion. Wengi wanatarajia kuwa baada ya miaka kumi ya MAC OS X, Lion, mfalme wa pori, itakuwa ndio toleo la mwisho la Mac OS X na hivyo tutarajie OS nyingine kabisa katika uwanja huu miaka michache ijayo.


Lion itaingia madukani mwezi wa Julai mwaka huu. Kilichowafurahisha zaidi watumiaji na washabiki wa Apple ni namna ambavyo OS hii itakavyouzwa kwa bei rahisi. Apple wameshusha bei kutoka Dola za kimarekani 129.00 hadi Dola 29.00. Punguzo hili linatosha kabisa kuondoa urari wa bei (inflation) katika sekta nzima ya kompyuta. 

Mac OS Lion inakuja na huduma mpya zaidi ya mia mbili. Hatuna budi kukiri kwamba haya ni mapinduzi kamili katika OS hiyo, ingetosha kabisa hata kuifanya kuwa ni OS nyingine badala ya kuwa ni toleo jipya la Mac OS X. Imabadilika kuanzia namna inavyoonekana hadi jinsi ya kuitumia.

Apple ambayo ni kampuni inayolenga faida zaidi katika vifaa kuliko software inaonekana wazi kuwa mafanikio yao bado kugonga kilele, kwani mauzo ya kompyuta zao yameongezeka katika kipindi cha nusu mwaka kwa 28%, ukilinganisha na PC ambapo mauzo yameshuka kwa 1%.  Bila ya shaka OS Lion itavutia zaidi wateja kununua kompyuta za Mac.

Miongoni mwa huduma mpya katika Mac OS Lion ni pamoja na Mission Control, auto save, Air Drop na Lauchpad. Huduma nyingine ni pamoja na kamusi, kuhamia kutoka kwenye kompyuta ya Windows na huduma ya taarifa muhimu katika matumizi (push notifications), ambayo ilikuwa ni huduma inayopatikana kwenye simu tu.
Vile vile itakapokuwa tayari kwa mauzo Mac Os Lion itauzwa moja kwa moja kwenye Mac App Store. Ina ukubwa wa gigabayti nne na ili kuweza kuitumia unatakiwa kuwa na kompyuta yenye Mac OS Snow Leopard. Kwa upande wa Developers tayari wao wameshaanza kuonja uhongo wa Lion kwani imetolewa kwao kuanzia jana. Tutaendelea na mfululizo wa makala hizi za wiki ya WWDC, na kuanza kuichambua Mac OS Lion katika kile tulichokiita huduma ya ‘Ishara za Miguso’, usiache kuchungulia chungulia kwenye blogi ya Gajetek.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s