iMessage ni ‘BBM’ ya Apple.

>

Huduma ya mpya ya iMessage ikielezewa kwenye WWDC 2011 
Blackberry Messenger maarufu BBM ni huduma ambayo imewavutia wengi kwenye simu za Blackberry na imetamba kwa muda mrefu sasa, ni huduma ya aina ya kipekee kwa watumiaji wa simu hizo. Sasa hawako peke  yao kwani iOS 5 imetolewa na huduma mpya ijulikanayo kama iMessage, Watumiaji wa vifaa vinavyotumia iOS yaani iPhone, iPod Touch na iPad wataweza kutumiana ujumbe kupitia vifaa hivyo.

Huduma ya iMessage inaletwa na utaalam wa hali ya juu. Mbali na ujumbe wa maneno watumiaji wataweza kutumiana video, picha na hata kutuma message hizo kwa kundi la marafiki badala ya mtu mmoja tu. Pia watumiaji wataweza kutumiana mafaili yanayofadhi anuani, nambari za simu na email za marafiki zao (Full contacts)

Ikiwa tayari inaonekana kuwa na ubora wa hali ya juu huduma hii ya iMessage pia itamuwezesha mtuma ujumbe kupata risiti inayomjulisha kuwa ujumbe wake umepokelewa na mkusudiwa, pia risiti nyingine inayomjulisha kwamba mkusudiwa tayari ameusoma ujumbe au kuangalia picha au video aliyotumiwa. Mbali na hilo mtuma ujumbe ataweza kujua kama mpokea ujumbe ameanza kujibu kabla hata jibu halijatumwa kwa hiyo ataweza kujua kama asubiri na mazungumzo yanaendelea.
Mbali na yote haya pia kwa wale ambao wana vifaa vya i (iDevices) zaidi ya kimoja wataweza kuseti kwamba mazungumzo baina yao na marafiki zao kwenye iDevice yaingie moja kwa moja kwenye vifaa vyote. Hii ina maana mazungumzo yote kwenye iMessage ambayo yamefanyika kwenye iPhone yako utayakuta tayari yako kwenye iPad yako bila ya wewe kufanya lolote zaidi ya kuseti kwamba iPhone na iPad ni vifaa vya mtumiaji mmoja kwenye akaunti ya iTunes.
Je hii itaiwacha wapi kampuni ya RIM inayotengeneza simu na tablet za Blackberry? Jibu ni kwamba iwapo wateja wa Apple wataweza kuikubali huduma hii ipasavyo basi maana yake ni kwamba RIM waanze kutafuta sababu nyingine itayovutia simu zao kwani BBM itakuwa si kivutio tena. Wengi wanadhani kuwa RIM wamezorota mno katika kuziendeleza au kuziboresha simu zao kwa vile kivutio cha mauzo ni BBM ambayo kwa muda mrefu huduma hii haina mpinzani. Iwapo RIM hawajajiweka vizuri na kuimarisha ubora wa Blackberry basi chini ya miaka mitano huenda tukatembelea kaburi la RIM na Blackberry zao. Kama vile MSN ilivyo mahututi hivi sasa na kama marehemu Hi Five alivyofariki kutokana na kuibuka kwa Facebook. Hata hivyo dalili nzuri kuwa huenda RIM wamepata somo kubwa katika simu zao zimejitokeza katika tablet yao mpya Blackberry  Playbook. Ni wazi kuwa RIM uwezo wanao kinachotakiwa ni ubunifu mahiri ili waendelee kuwepo mchezoni.
Huduma iMessage itafanyika kupitia mtandao wa WiFi na 3G (au GSM) yaani kama unatumia WiFi maana yake itakuwa bure na kama unatumia 3G maana yake itachukua kiasi fulani cha internet yako ya 3G, au wale wenye simu na iPad 3G za mkataba (Contract) ni bure moja kwa moja. Hivyo basi watumiaji wa iPhone na iPad 1 na 2 zenye 3G wao wataweza kutumia huduma hii wakati wote lakini wale ambao wana iPad zisizo na 3G na iPod Touch watalazimika kuwa katika sehemu zenye WiFi ili kuweza kutumia huduma hii. iMessage ni moja kati ya huduma 200 mpya zinazopatikana kwenye iOS5 ambayo inatekemewa kutoka miezi michache ijayo kwa wateja wakati kwa Developers (watengeneza Apps)  imetoka leo.


Huduma hii itakuwemo kwenye iPhone 4, iPhone 3GS, kizazi cha 3 na cha 4 cha iPod Touch pamoja na iPad zote mbili. Iwapo una iPhone 3G au iPhone na iPod touch kizazi cha kwanza au cha pili basi simu au iPod yako haitakuwa na huduma hii.
Kaa mkao wa kula kwani wiki nzima au hata zaidi tutazungumzia yale yanayojiri WWDC 2011 (Mkutano wa Apple na Developers wao) moja kwa moja kutoka San Fransisco. 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s