Sony NGP kuitwa PS Vita

>

Kizazi kijacho cha PSP kikiwa na jina muda tu la NGP (Next Generation Portable) huenda jina lake halisi itakapoanza kuuzwa likawa ni Playstation Vita. Habari hizi zimetolewa na wadau wa gajet ambapo Sony kwa bahati mbaya walisahau kufuta jina hilo walipopeleka kifaa hicho kupasishwa. Bila shaka Sony hawatapendezeshwa na kuvuja kwa jina hili, je Sony wataliacha au kulibadilisha? Jibu litapatikana mwezi Disemba gajet hii itakapotolewa rasmi kwa mauzo.


Tukiachana na jina, konsoli hii itakuwa na skrini ya kugusa yenye ukubwa wa inchi 5 ikiwa piksel 960×544 aina ya OLED. Mambo mengi katika konsoli hii ni mawili mawili. Inakubali ‘touch’ kwenye skrini mbele na kwenye bazel ya nyuma, ina kamera mbili, ina spika mbili, ina prosesa yenye core mbili na ina analogue stick mbili, moja kulia na nyingine kushoto.
Mbali na viwili viwili prosesa yake ni aina ya ARM Cortex A9 na betri inadumu kati ya masaa manne hadi matano. NGP inategemewa kutoka ikiwa na vivutio vingi. Moja kati ya mambo ambayo Sony imetangaza ni kwamba konsoli hii itatoka ikiwa na game zenye kiwango (quality) cha PS 3. Ikiwa hili ni sahihi na kuzingatia udogo wa skrini ukifananisha na TV, basi haya ni mafanikio makubwa. Kivutio chingine ni kule kuweza kutumia bazel ya nyuma kucheza game. Hivyo basi konsoli hii itakuwa ni yenye namna nyingi za kuitumia kuliko konsoli zote za mkononi. Skrini ya kugusa, analogue stick mbili, bazel ya nyuma pamoja na vifungo vya digital vinane. NGP itakuwa na WiFi, 3G, Bluetooth, accelerometer pamoja na GPS.
Kiteknolojia konsoli hii itakuwa imekamilika, itatumia memory stick badala ya disk aina ya UMD ambapo inaonekana kwamba Sony wameamua kuachana nazo moja kwa moja, UMD zimekosa umadhubuti na hivyo kuwatia hasara watumiaji kutokana na kuharibika kwa haraka. Pia ni zenye kupoteza nafasi na kuongeza ukubwa wa gajet ukilinganisha na uwezo mkubwa ambao memory kadi iliofikiwa kwa sasa na ukizingatia udogo wa kadi hizo. Hata hivyo ngoja ya konsoli hii itaumiza sana matumbo kwa vile kuna miezi karibu sita ya kusubiri. Sony bado hawakutangaza bei ya NGP. Wapenzi wa gejet tayari wameshaanza kujiuliza watakuwa na gajet ngapi zenye kutumia sim card. Simu, tablet na sasa konsoli ya mkononi. Hatujui nini kitafuatia.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s