Kogan Agora laptop ya kwanza ya Chromium OS

>

Kampuni ya Australia Kogan imekuwa ya kwanza kutoa laptop inayotumia OS ya Google Chromium kwa mauzo. Laptop hii kwa viainisho halisi inachosha. Kwanza inatumia prosesa yenye kasi 1.3 Ghz aina ya celeron, kama bado hujachoka ina RAM 1GB na nafasi ya kuhifadhia mafaili ni 30GB tu, aina ya disk ni SSD. Hakuna mengi ya kueleza kuhusu laptop hii, faraja kubwa inapatikana kutokana na  bei nafuu, nchini Uingereza bei ya laptop hii ni £269.00 (Tsh. 684,209.00) Mbali na vianisho hivi laptop hii pia ina skrini yenye ukubwa wa inchi 11.6, betri yake inadumu masaa matatu na nusu pia ina  webcam, bluetooth na HDMI port.
Ingawa ina vianisho kama kwamba ni ya mwaka 2005, OS mpya ya Google Chromium huwawezesha watumiaji kuhifadhi mafaili online kupitia huduma ya cloud. Kwa yoyote mwenye hamu ya kujaribu Google Chromium laptop hii inatinga madukani wiki ijayo, usije ukasahau jina, ni Kogan Agora. 

Wengi wanadhani OS ya Google Chromium inawakilisha hali halisi ya utumiaji wa kompyuta ya miaka ijayo. Hii ni kwa sababu programme zote kwenye laptop hii zinaweza kuhifadhi mafaili moja kwa moja kwenye mtandao na hivyo kurahisisha kuyapata tena mafaili yako popote bila ya kujali unatumia kompyuta ipi, ili mradi pawe na intanet, vile vile hata program zenyewe zinatumika kutoka mtandaoni. Kama huna internet ya uhakika basi kwa sasa sahau kuhusu laptop yoyote yenye kutumia OS hii.
Kwa upande mwingine OS ya Chromium bado ni changa na ni mapema mno kuweza kujua kama itakubalika na watumiaji au laa. Kwa watengeneza kompyuta OS hii inavutia kwa vile ni open source. Hata hivyo Linux Ubuntu ni OS ya open source ambayo imekuwepo kwa muda mrefu sasa lakini bado kuwa ni yenye kutumika na wengi. Muhimu ni kwamba Chromium imetolewa na Google, kampuni ambayo imepata mafanikio katika bidhaa mbali mbali ikiwa ni pamoja na Android ambayo kwa sasa ni OS ya simu yenye kuuza kwa wastani simu 350,000 kwa siku.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s