Pagani Zonda Tricolore

>

Hii ni supercar iliyotengenezwa na Kampuni ya kitaliana Pagani Mobili ambayo pia hutengeneza ndege za kivita. Jina la gari hii ni Pagani ambalo ni neno la Kitaliana lenye maana ile ile ya kiswahili (Upagani), yaani kutomuabudu Mungu mmoja. Tricolore maana yake ni mionzi yenye rangi tatu. Kwa nini kampuni na gari hii imeitwa Pagani? Hili hawalielezi wazi wazi lakini tunachojua sisi ni kuwa hata kasi yake ni ya kipagani na bei yake ni ya kipagani ambayo inakaribia $1,000,000.00 (sawa na Shilingi za Tanzania Bilioni 5.5). Pagani Zonda Tricolore ina uwezo wa kutoka 0 mpaka 100 kph kwa sekunde 3.4. na 0 hadi 200 kph kwa sekunde 9.6. Ni kasi inayozidi baadhi ya gari zinazoshiriki kwenye Formula 1. Pia gari hii ina injini ya Mercedes Benz AMG ile ile iliyotumika kwenye Gari inayoendeshwa na madereva wawili tu kwa sasa nao ni Lewis Hamilton na Jenson Button, yaani madereva wa timu ya Formula 1, Vodafone Mercedes McLaren, inayoshikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo hivi sasa. Hii kitu si mchezo.
Injini ya gari hii pia ina nguvu za ‘hospawa’  670. Ina gia boksi aina ya Cima Sequential (gia 6) ambayo hujibadili wenyewe, gia hii ina teknolojia ya ‘robotic’. Maringi ya mbele yana ukubwa wa 9×19 na yale ya nyuma 12.5×20 na kuifanya supercar hii iwe na mbinuko wa aina yake. Ina breki aina ya brembo iliyochanganya teknolojia ya carbo-ceramic na hydrolic servo. Ina uzito wa kilo 750 tu. Pamoja na wepesi huu ina downforce ya 300 kph kwa hiyo unaweza ukakunja kwa kasi ya hali ya juu bila ya kupinduka. Hii pia inatokana na kuwa na uzito mkubwa nyuma kuliko mbele.  

Shoko mzoba (Shock absorber) zake zimetengenezwa kwa mchanganyiko wa madini ya magnesium na titanium ambayo huzifanya kuwa na umadhubuti wa hali ya juu. Gari hii haifai kabisa kuwa katika nchi zenye barabara ambazo zina mashimo kwa vile uvungu wake ni mdogo mno au tuseme iko chini sana. Supercar hii imetoka mwaka 2010.
Kutokana na ughali wake gari hii huendeshwa na watu wachache sana ulimwenguni, na hivyo kuna nchi nyingi tu ambazo gari hii hutaweza kuiona kwa macho, tungekushauri uitazame picha yake kwa makini kwa vile huenda usiione tena maishani mwako, ni Pagani Zonda Tricolore.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s