Tungependa iPhone 5 Iwe…

Tungependa iPhone uwe kama kwenye picha hii
Yafuatayo ni mapendekezo ya Gajetek juu ya nini kipya au nini kiboreshwe kenye iPhone 5, katika orodha yetu hii tutaweka vile ambayo tunahisi vitairudisha iPhone kwenye hadhi yake ya kuwa ni simu bora kuliko zote Duniani na yenye kuvutia na kuleta raha unapoitumia. Orodha yetu itachanganya vile ambavyo tunatarajia kutekelezwa na Apple kadhalika na vile ambavyo Apple kwa sababu moja au nyingine hawatavitekeleza.

Tungependa kuona teknolojia ya NFC kwenye iPhone 5. Hili ni jambo ambalo sisi hatutarajii kuwa Apple watalifanya kwa vile bado haliko wazi ni vipi litawanufaisha Apple, ingawa manufaa kwa wateja ni makubwa, hebu fikiria, gari yako unaiwasha kwa simu badala ya ufunguo na ukienda dukani unalipa kwa iPhone badala ya kadi ya benki au fedha taslimu.

Prosesa ya Dual Core: Ingawa iPhone 4 ina kasi ya kutosha tungependa kuona kasi kwenye simu hii inaongezeka kwa kutumia prosesa hii. Hili Apple wanaweza kulifanya au kulipuuza kwa vile iPhone haina matatizo ya kasi.
Tungefurahia mno kuona iPhone 5 ina uwezo wa kutumia flash. Kwa kweli hii ni kero nambari moja ya simu za iPhone. Hili kamwe Apple hawatalitekeleza kwa vile ni teknolojia ya wapinzani wao (Adobe). Na pia Apple wanahofia kuharibu mauzo ya App Store na hasa kwenye masuala ya Games, kwani website nyingi za game zinatumia flash.
Kamera: Iwe na angalau megapiksel 8 na uwezo wa kurekodi video za 1080p. Hili tunalitarajia mno katika iPhone mpya, simu mbali mbali kama vile Samsung Galaxy S2 na Sony Ericsson Experia Arc tayari zina uwezo huu.
Tungependa kuona skrini yenye ukubwa wa inchi nne au nne nukta tatu badala ya tatu nukta tano. Hili hatutarajii kwamba Apple watalifanya kwa vile Steve Job aliwahi kueleza kwamba wanadhani simu yoyote yenye ukubwa zaidi ya iPhone basi imepindukia mpaka.
Tungependa kuona jina tofauti na iPhone 5. Kuiita simu 4, 5 au nambari yoyote kwa kweli haisisimui. Hili halitatekelezwa kwani Apple wakishakuweka ‘i’ mwanzo hawana tena jingine kwenye mambo ya majina tofauti na HTC ambao hushusha majina ya kusisimua kama vile Chacha, Salsa na Sensation. Kwa mfano iPhone Brilliant au iPhone Kiraka.
Tungependa iwe na umbile tofauti na iPhone 4, zaidi ifanane na iPad 2. Hili tunatarajia Apple watalitekeleza hasa ukizingatia kashfa ya “Antenna gate” iliyomuumiza kichwa sana Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hii, Steve Job mpaka kufikia kutoa Bumper za bure kwa wateja walionunua iPhone 4 mwanzoni.
Pia tungefurahia iPhone 5 iwe na iOS mpya kabisa iliyoboreshwa na kubadilishwa kiasi kikubwa ili ujihisi kuwa na simu tofauti. Hili tunalitarajia ukizingatia kwamba mkutani ujao ni wa kutangaza OS mpya.
Tungependa Apple watupe mshangao mwingine kwa kuingiza kwenye simu hii teknolojia ambayo hatukuitarajia. Hili tulitegemee sana, kama Apple walivyotoa Retina Display kwenye iPhone 4 au Magic Cover kwenye iPad 2. Kwa mfano skrini yake iwe haivunjiki hata ukiipiga jiwe, au teknolojia yoyote nyingine ya ajabu ajabu.
Tungependa iPhone 5 iwe nyembamba zaidi na nyepesi zaidi kuliko matarajio yetu. Hili linawezekana kwani kukondesha bidhaa ni moja kati ya kawaida ya Apple. Milimita 8 tosha.
Betri idumu zaidi kuliko ile ya iPhone 4. Hili pia ni jambo ambalo halitotushangaza kwani katika masuala ya kuboresha nguvu za betri Apple wametia fora.
Iwe na uwezo wa ku-sync na iTunes bila ya kuunganisha na waya (wireless syncing) Hili ni ‘big no’. Kwanza watapoteza milioni chache za kuuza waya pili haitakuwa na maana kwa sehemu za ulimwengu ambazi internet haina kasi sana. Lakini sehemu kama vile Korea ya Kusini ambapo internet imeshafikia kasi ya 1000 mbps (kasi ya juu Uingereza ni 100 mbps) Macho kuvimba watalifurahia hili.
Bei ipungue, hili pia haliwezekani kwani Apple wanaona fakhari kuuza ghali bila ya kujali kipato na hali. Vile vile iwe na skrini ya 3D bila ya miwani. Hili n’go Apple hawalifanyi kwani wao si wenye kuvamia teknolojia mpya kabla haijawiva vizuri.


Tungependa iPhone 5 iwe na uwezo wa kuhifadhi mafaili zaidi, hii tunamaanisha kwamba iwepo yenye uwezo wa 64GB, hili si kubwa kwa Apple kwani tayari kuna iPod touch yenye uwezo huu, hata hivyo imekuwa ni utamaduni wa Apple kuwa na iPod Touch yenye uwezo kuliko iPhone, hii maana yake Apple hawatatoa iPhone yenye 64 GB mpaka watakapoamua kutoa iPod Touch yenye 128GB. Kutokana na ughali wa aina za disk zinazotumiwa kwenye gajet hizi, yaani Solid State Drive (SSD) hili hatuna unakika nalo kama Apple wako tayari.
Mengi kati ya ambayo tungependa kuyaona yatabaki kuwa ndoto, na wewe ndugu msomaji tuandikie katika comment ungependa iPhone 5 iwe na nini. 
Advertisements

One thought on “Tungependa iPhone 5 Iwe…”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s