Microsoft Wazindua Windows 8

 

Kiangazi kinakuja na ushindani wa kibiashara katika gajet unapamba moto, Microsoft wamefanya uzinduzi na kuonesha OS yao mpya ambayo imeitwa Windows 8, siku 4 tu kabla Apple nao kuzindua rasmi OS zao yaani Mac OS Lion na iOS 5. Dalili za awali zinaonesha wazi kuwa Microsoft wamerudi mchezoni kwa nguvu zote, na hasa katika  kompyuta za tablet.

Iwapo unataka kuielezea Windows 8 kwa kifupi basi ni mchanganyiko wa Windows Phone 7 ambayo ni OS ya simu na Windows 7 ambayo ni kompyuta. Wakati matarajio ya wengi ilikuwa kwamba Windows 8 itakuwa ni kwa ajili ya tablet na kwa hiyo UI (User interface) kwa ajili ya skrini za multitouch, Microsoft pia wametangaza kuwa OS hiyo itatumika kwenye kompyuta na tablet vile vile, OS hii itaweza kuendesha programu zote zinazotumika kwenye Windows 7.
Ikiwa na interface ya Touch, Windows 8 inatumia tiles badala ya icons kama tulivyozoea kwenye Android na iOS. Tiles zinaonekana kuwa na ubora zaidi kwa vile skrini za tablet ni kubwa kulinganisha na zile tales za Windows Phone 7 ambapo zinabanwa kutokana na udogo wa skrini za simu. Maoni ya wadau wengi ni kwamba Microsoft ‘wamecheza kama Pele’, yaani unapotaka kula maisha unaweza kutumia UI ya touch kwenye tablet yako na unapokuwa na kazi za muhimu basi unaunganisha kibodi na mouse ili kuitumia kama kompyuta. Hivyo basi tablet za Windows 8 zitakuwa ni za pili kutoa suluhisho la kutumia tablet kwa kazi muhimu kama vile spreadseet, wordprocessor, publisher au Presentation, ingawa iPad nayo ina uwezo kama huu si wengi wenye kutumia ipad kwa shughuli za kompyuta lakini badala yake huwa inatumika kwa madhumuni ya tablet.
Unapobadilisha UI na kuweka ya kompyuta, inaonekana kama ni Windows 7 kwa kila namna isipokuwa tu Windows 8 pia inachanganya UI zote mbili kwa wakati mmoja na inaonekana kufanya vyema kabisa katika masuala ya multi tasking na multi touch. Namna ilivyobuniwa ni kwamba inavutia mno na ni lazima tukiri kuwa wa wataalamu wa Microsoft. wamefanya ubunifu wa hali yajuu. Microsoft ilionekana kuzorota kidogo katika kipindi cha kiasi miaka Mitatu nyuma, kutokana na ukweli kwamba Windows Mobile 6.5 ilionekana kuwaboa watumiaji na kadhalika Windows 7 ilionekana si yenye kuvutia kwenye tablet kwa vile haikutengenezwa kwa ajili ya skrini za kugusa. 


Wachambuzi wanaamini kuwa sio tu kwamba OS hii itapunguza ukiritimba wa Android katika kompyuta za tablet lakini pia itatoa ushindani wa hali ya juu ukizingatia kwamba mambo mengi ambayo kwenye Android yanafanywa na Apps kwenye Windows ni sehemu ya OS, hivyo basi huna haja kulipa lipa pesa mara kwa mara kwa ajili ya kuiongezea tablet yako kufanya mambo madogo madogo kama vile twitter na facebook.

Baadhi ya kampuni kama vile Acer tayari zimeanza kutoa malalamiko juu ya masharti magumu yaliyowekwa katika hardware ili iruhusiwe kutumia Windows 8, Microsoft wametoa vianisho halisi vya hali ya juu ili kuhakikisha kwamba tablet hizo zinatoa ushindani wa hali juu katika masuala ya viwango (quality). Wakati kwa wazalishaji kuna malalamiko kwa upande wa wateja wategemee kupata tablet zenye umahiri na ubora wa hali ya juu. Ni vigumu kuelezea uhondo wa OS hii kwa hiyo basi chungulia kwenye video klip hapo chini ii upate picha halisi ya Windows 8 hii. Ila wadau wanajiuliza ni vipi utaweza kutumia UI ya tiles kwenye kompyuta ambayo haina touch skrini? 


Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s