iWork ya iPhone Yatolewa

 

Kampuni ya Apple imetoa apps za iWork kwa ajili ya iPhone na iPod touch. iWork ni kama Microsoft Office kwa kompyuta za Mac. Tayari Apple walishatoa apps hizi kwa ajili ya iPad. iWork huwa na Apps tatu ambazo ni Pages, Keynote na Numbers.
Pages ambayo ni word processor sawa na Microsoft Word katika package ya Office. Numbers kama inavyojieleza ni spreadsheet kwa ajili ya masuala ya mahesabu na App inayohusika na masuala ya presentation ni Keynote. Pia iPhone na iPod Touch zina app ya rimoti ya kuendeshea Keynote kwenye kompyuta za Mac na iPad kwa ajili ya kufanyia presentation, lakini rimoti hii huuzwa mbali.

Faraja kubwa ni kwa wale ambao wameshanunua Apps hizi kwenye iPad kwani wao wanaweza ku-download bure kabisa kwa sababu zimeambatanishwa kama bidhaa moja kwenye App Store, kwa hiyo kama una iPad na ulinunua Apps hizi tinga kwenye iTunes au App Store na u-dwonload bila ya kulipa tena.
Iwapo hujanunua Apps hizi basi kila moja inagharimu £5.99 (sawa na TSh 15,234.00) kwa hiyo jumla ni TSh 45,700 kwa Apps zote tatu.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s