Apple kuzindua iPhone Mpya?

 

Tarehe 6/6/2011 ndio siku, asiye na mwana aelekee jiwe, ni siku ambayo kampuni kubwa na mahiri kabisa ulimwenguni, Apple imetangaza mkutano ujulikanao kama Worldwide Developers Confarence (WWDC 2011) utaanza na kufanya uzinduzi wa bidhaa zake mpya kadhaa. Tayari wanahabari, wachambuzi na wapenda gajet ulimwenguni kote wameshaanza kumiminika katika kitongoji cha Moscone West, San Fransisco CA kwa ajili wa uzindunzi na mkutano huo, sisi wa Gajetek tunawaahidi washabiki wetu kuwa tutakuwa ‘live’ kukuchambulieni bidhaa hizo katika blog yetu. pamoja na kwenye twitter (@gajetek) yetu. Tiketi za mkutano huo tayari zimemalizika na katika mnada wa mtandaoni eBay tiketi hizo zimekuwa zikilanguliwa kwa hadi  $3,500.00Pamoja na usiri mkubwa ambao Apple huufanya kabla ya uzinduzi huo Gajtek imedokezwa na wadau kutoka ndani ya Apple kuwa miongoni mwa bidhaa zinazotarajiwa kutangazwa ni ama iPhone 5 au iPhone Nano, Mac OS Lion ambayo ni operating system mpya ya computer za Mac, iOS 5 (operating system mpya ya iPhone, iPod Touch na iPad) ambayo itatolewa bure kwa wote wanaomiliki gajet hizi. Pamoja na bidhaa hizi pia Apple wanatarajiwa kutangaza huduma mpya ya muziki aina ya Clouds, hii inaonekana ni kati ya mikakati ya Apple katika ushindani wa kibiashara. Hivi karibu kampuni za Google na Amazon zimetangaza huduma sawa hii. Hata hivyo habari rasmi za Apple hazikutaja kabisa kama iPhone itazinduliwa. Tayari Apple wanatoa huduma ya kuhifadhi mafaili katika mtandao ambayo haina muziki ambayo ni Mobile Me.
Sisi katika Gajetek tukiwa tumebahatika kutumia Mac OS Lion beta version tunaamini kabisa kuwa OS hiyo ina ubora wa hali ya juu, tunadiriki kusema kuwa ni nambari moja ulimwenguni kwa sasa, kwa hiyo iwapo Microsoft wanalenga kutoa ushindani katika OS, basi hawana budi kuiboresha mno Windows 7 na labda kutoa nao kutoa Windows mpya kabisa. Kwa sasa Microsoft wametangaza kuwa watatoa Windows 8 ambayo ni kwa ajili ya tablet tu.

Lakini kinachosubiriwa kwa hamu zaidi na washabiki wa Apple, ambapo watafiti hivi karibuni wamesema kuwa kampuni hiyo imekuwa na athari kwa baadhi ya watu kama ile athari inayopatikana kwenye dini kwa waumini, ni simu ya iPhone mpya. Kwa kawaida kampuni hiyo inapotoa simu mpya hijikita kwenye kilele cha simu bora Duniani, ni mwezi uliopita tu ndio iPhone 4 imeng’olewa kileleni na Samsung Galaxy S2. Hivyo basi wengi wanadhani kuwa ni wakati muafaka kwa iPhone mpya kutowela. Apple hutoa iPhone moja tu kila mwaka lakini mwaka, tofauti na kampuni nyingine ambazo hutoa simu kadhaa kwa mwaka.

Mbali na kutangaza bidhaa mpya, Apple pia watatoa takwimu zitakazoonesha mauzo ya bidhaa mbali mbali katika kipindi kilichopita, wengi wana hamu ya kujua mafanikio ya iPad 2, je yatakuwa ni kama yale ya iPad? Wachambuzi wanatarajia kuwa mauzo ya iPad 2 hayatakuwa makubwa kama yale ya iPad kwani bidhaa mbili hizi hazikutofautiana sana kiasi cha kuwafanya wenye iPad kununua iPad 2, kadhalika mwaka kumekuwa na tablet nyingi mbadala zenye ubora ambazo watu wamekuwa wakinunua kama vile HTC Flyer, Blackberry Playbook, Motorola Zoom na Acer Iconia. Vile vile wengi wana hamu ya kumuona Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Steve Jobs ambaye amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani (cancer) katika Pancreas, mara ya mwisho alipojitokeza hadharani Steve Jobs alionekana kudhoofika kwa kiasi fulani.
Stay tuned katika Gajetek, tarehe 6 mwezi wa 6 tutablog moja kwa moja yatakayojiri Moscone West, San Fransisco CA. Mkutano huo utafanyika kwa muda wa siku 5 lakini ni siku yamwanzo tu ndio kutakuwa na uzinduzi, zilizobaki developers wataoneshwa namna ya kuziendeleza iOS na Mac OS X. Pia kama tulivyosema huko juu unaweza kutufuatilia katika twitter siku hiyo @gajetek ndio twitter address yetu.
Advertisements

One thought on “Apple kuzindua iPhone Mpya?”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s