>Soka Na Teknolojia

>

Leo ni leo, asiye na mwana aelekee jiwe, ama Man U au Barca. Ni siku ya fainali ya ligi ya Mabingwa wa Ulaya ambapo mabingwa wa nchi mbili zinazotawala katika soka Duniani Uingereza na Uspanyola watapambana. Sisi katika Gajetek tunaangalia mchezo huu na teknolojia.
Chips za GPS katika Mpira wa Adidas. 
Teknolijia ya mstari wa goli, hii ni teknolojia ya kuwasaidia waamuzi kujua kama mpira umevuka mstari wa goli kwa hiyo goli limeingia au haukuvuka. Kwa muda mrefu sasa viongozi wa shirikisho la soka duniani FIFA kwa  nguvu zote wamekuwa suala la wakipinga teknolojia yoyote kutumika ili kumalizo mzozo huo ambapo mara kadhaa waamuzi hutoa uamuzi usio sahihi kama goli au si goli, kosa maarufu la namna hii ni lile lililofanyika katika Kombe la Dunia Afrika ya Kusini mwaka jana. Kiungo wa Uingereza Frank Lampard, alipopachika bao katika mechi dhidi ya Ujerumani na muamuzi alishindwa kujua kama mpira ulivuka chaki ya goli. Kwa nini Blatter na viongozi wenziwe wamekuwa wakipinga matumizi ya teknolojia kuwasaidia waamuzi katika suala hili? Wengi kati ya wapenzi wa mchezo huu maarufu Duniani kwa kweli hawakubaliani na hoja dhaifu anazotoa rais huyu wa shirikisho la soka, kama vile eti matumizi ya teknolojia yatapunguza ladha ya mchezo! Tuachane na Blatter ambaye huenda ana ajenda za siri katika hili, muhimu kwetu sisi ni teknolojia.

Teknolijia ya mstari wa goli ipo tayari, kinachosubiriwa ni FIFA kuidhinisha majaribio na hivyo iweze kutumika msimu ujao, hata hivyo FIFA bado hawajatoa kauli thabiti. Mipira itaingizwa kifaa cha GPS (Geographical Pisitioning System) ambacho kina uwezo wa kujua mahala ambapo mpira upo popote uwanjani kwa kutumia satalaiti maalum na kwenye mstari wa goli panawekwa lesser beam ambazo zina vihisia (sensor) vinavyoweza kuwasiliana na chip ya GPS iliyoko kwenywe mpira kwa hiyo iwapo mpira utavuka kwenye mstari wa goli lesser beam zitaweza kumjulisha muamuzi kuwa mpira umevuka chaki ya goli hivyo kuondoa makosa ya uamuzi katika suala hili.
Texaco Shinpads zenye sensors 
Mbali na teknolojia hii, hivi karibuni kampuni ya Texaco wametengeneza vikinga ugoko (Shinpads) vyenye uwezo wa kumjulisha muamuzi kama mchezaji amechezewa rafu au amejitupa. Vikinga ugoko hivyo vimewekewa vihisia (sensors) maalum ambavyo vinauwezo wa kutambua iwapo mchezaji amegongwa kweli au amejitupa tu. Iwapo amegongwa vihisia hivyo vitampelekea habari muamuzi kuwa rafu ni ya kweli, la kama hakugusana na mchezaji mwenziwe vihisia hivyo havitatoa mawasiliano yoyote na hivyo muamuzi atajua kwamba mchezaji amejitupa. Baadhi ya washambuliaji katika soka wamekuwa na tabia ya kujitupa katika boksi ya 18, ili kumhadaa mwamuzi kutoa penalti. Muamuzi mstaafu maarufu wa soka Uingereza Jeff Winter ameeleza kufurahishwa kwake kutokana na kutengenezwa kwa shinpads hizo kwa vile zitatoa msaada mkubwa kwa waamuzi. Je FIFA watazuia na hizi? 
Sisi katika Gajetek tunawatakia wapenda soka fainali njema, timu yetu ni itakayoshinda, hivyo tuna uhakika Mungu akipenda, timu yetu leo inachukua ubingwa. Ingawa mara nyingi inatubidi kubadili timu, faida yake ni kwamba mara zote tumo furahani. 
Advertisements

2 thoughts on “>Soka Na Teknolojia”

  1. >Nadhani ni mambo yanayohusiana na kamari za matajiri, hili huwawezesha wao kumfanya refa apendelee, teknolojia yoyote ambayo itamnyan'ganya refa uwezo wa kufanya upendeleo basi FIFA huwa hawaikubali.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s