>Kwa Nini Blackberry Haziingii Kwenye 10 Bora?

>

Nembo ya Blackberry simu maarufu kutokana na BBM

Kumi bora mara nyingi huwa ni mtazamo binafsi wa mwandishi au kundi fulani, hata hivyo ukiangalia chati za simu kumi bora mbali mbali zenye kutofautiana, kuna kitu kimoja zinafanana, nacho ni hakuna simu za Blackbery. Kwenye makala hii tutajaribu kufanya uchambuzi wa kina juu ya sababu zinazopelekea simu hizo kutokuwemo kwenye chati.Blackberry ni simu zilizopata umaarufu mkubwa na kutumiwa na wateja wengi Duniani. Simu hizo hutengenezwa na kampuni iliyopata mafanikio katika sekta hii ijulikanayo kama Research In Motion maarufu zaidi kwa ufupisho wake, RIM. Pamoja na umaarufu wa simu hizo ni mara chache sana kuona simu za Blackberry zinaingia kwenye chati ya simu 10 bora. Kwa mfano tangu mwaka 2010 hadi sasa ni Blackberry Torch pekee ndiyo iliyoingia katika chati hiyo ambao inatawaliwa na simu za Apple, HTC na Samsung. Hata Blackberry Torch ilikaa kwa muda mchache na kutolewa.
RIM, nembo ya kampuni inayotengeneza simu za
Blackberry, Research In Motion
Ubora wa Blackberry
BBM: Simu hizi zimejipatia umaarufu mkubwa kutokana na kuwa na njia ya kutumiana ujumbe baina watumiaji wake ijulikanayo kama Blackberry Messenger (BBM) ambapo wateja hupeana Blackberry Pin (BBP) na kuweza kuwekana katika orodha ya wenye kutumiana ujumbe, vile vile mtumiaji anaweza kumuingiza mtumiaji mwenziwe katika BBM kwa ku-scan barcode yake iliyoko kwenye simu hizo. BBM imesababisha simu za RIM kupata umaarufu mkubwa miongoni mwa vija wa rika kati ya miaka 15 – 40 ukizingatia kwamba tumo kwenye wakati ambao mitandao ya kijamii au kibashasha (social network) ni kivutio kikubwa.
QWERTY kibodi: Hii inaendena sana na BBM kwa vile wengi wa watumiaji wa Blackberry huwa ni waandishi zaidi kuliko wazungumzaji katika simu zao, kibodi huwasaidia kuandika kwa kasi na urahisi kutokana na ufanisi mkubwa uliotumika na RIM kuzibuni (design) kibodi hizo.
Usalama (Security): Vile vile simu hizo zina usalama wa hali ya juu kwani si rahisi kwa mapaparazi, wapelelezi  au mahaka (hackers) kuweza kupata ujumbe kwa njia ya wizi kwa vile Blackberry inatumia mitandao yao wenyewe kama njia za kupeleka ujumbe. Hata imefikia baadhi ya serikali kutaka kupiga marufuku simu hizo kwani hata vyombo vya usalama vya nchi vilishindwa kupata kusoma BBM za watu wakihofia kwamba magaidi watatumia uchochoro huu kuweza kuwasiliana na hivyo kuhatarisha usalama wa nchi zao. Hii imeplekea watu wenye usiri kuvutiwa sana na simu hizo ikiwa ni pamoja na wanasiasa, wasanii na ‘masupastaa pamoja na maselebriti’ wengine.
QNX OS: Blackberry inatumia OS zao wenyewe ambazo hutumia utaratibu wa QNX. OS hii ina uwezo mkubwa wa kufanya mambo mengi sambamba (multi tasking) kwa namna ya kipekee, pia ina ufanisi wa hali ya juu kwa namna inavyofanya kazi. Muhimu zaidi ni kwamba Blackberry OS haihitaji kifaa (hardware) chenye kasi sana kufanya kazi kwa kasi, kwani OS hii ni nyepesi (lightiweight) mno.
Maradhi (Addiction): Utafiti unaonesha kwamba watumiaji wengi (si wote) wa Blackberry wana maradhi na simu zao kwa kuzitumia zaidi kuliko watumiaji wa simu nyingine zozote. Ukianza kutumia simu hizi basi ni taabu kuziacha, hali hii inachangiwa zaidi na BBM ambapo wengi wanapoitumia utadhani akili zimewaruka huwa hawasikii wala hawasikilizi, hucheka pekee yao na hujihisi hawako wapweke. Kwa upande wa RIM hili ni zuri kwani inakuwa si rahisi kumpoteza mteja.
Sehemu ya juu ya Blackberry Pearl 3G, ikionesha kamera yake
Udhaifu wa Blackberry
Zifuatazo ndio sababu za msingi zinazozifanya simu za blackberry kutokuwemo katika chati ya simu bora Duniani pamoja na kuwa na ubora tulioueleza mwanzoni:- 
Skrini: Kwa asili simu za Balckberry zina skrini ndogo ukifananisha na simu ambazo hutamba kwenye kumi bora. Simu zote zilizokuwa kwenye kumi bora kwa sasa zina ukubwa wa skrini  baina ya inchi 3.5 na 4.3. Bila ya shaka kampuni ya RIM wanalifahamu hilo ndio maana wakajaribu kutengeneza simu kama vile Torch na Storm. 
Ubora wa Skrini (Quality): Rizolushan (Resolution) ni za hali ya chini kwa mfano Blackberry curve ina rizolushan 320X240, hii husababisha simu za Blackberry kutokuwa na mvuto wala mng’aro kwenye skirni kama zilivyo simu ambazo zinakuwemo kwenye kumi bora. Itakuwa si sahihi kulinganisha iPhone 4 na Curve kwa hiyo hebu tuangalie iPhone 4 ambyo ndiyo simu inayoweka viwango na Torch. iPhone 4 ina rizolishan 960X640 na PPI (pixel per inch) 326. na BB Torch ina rizolushan 480X360 na PPI 187.5, kwa mapana na maferu tunaweza kusema kwamba hii ni aibu kwa RIM. Skrini huchukuliwa kuwa ni hali ya juu (high end) ikiwa na PPI 300 na ya hali ya chini (low quality) ikiwa na PPI 150 au pungufu. Hii itakupa picha ni vipi Blackberry wanabana matumizi katika masuala ya Skrini.
Bofa Skrini: Wakati simu za skrini za kugusa (touch screen) zinaingia na kupata umaarufu kuanzia miaka ya 2007 ilipotoka iPhone, RIM wakataka kujitofautisha na kutoa skrini za kubofa (click screen) badala ya kugusa, hii iliwaangusha vibaya kwani simu hizo hazikuweza kukubalika na wateja, athari yake katika makosa kama haya yamepelekea jina la Blackberry na RIM (brand name) kushuka thamani kwa 20%, (Chanzo WPP). Sasa linganisha na Apple watengezaji wa iPhone  ambapo brand yao imekuwa kwa 84% (Chanzo WPP)
Umbile: Nadhani hata baadhi ya watumiaji wa Blackberry watakiri kwamba simu hizi hazina maumbile ya kuvutia ukilinganisha na simu za Samsung, Apple, LG, Sony Ercisson na HTC. Hii imechangiwa zaidi na utaratibu wa RIM kuwa ni muhimu kwao kuweka QWERTY kibodi. Iwapo RIM wanataka kutoa ushindani katika simu za hali ya juu basi hawana budi kuwafukuza kazi baadhi ya wabunifu wa maumbile (designers) wao na kuajiri wapya.
Vianisho Halisi (Specs): Hapa hatuna maelezo mengi tutalinganisha Blakberry bora kuliko zote kwa viainisho (Torch) na Samsung Galaxy Ace ambayo ndiyo ya mwisho katika kumi bora za mwezi huu:
Torch: CPU 624 MHz, Kamera 5 mp, Video VGA 24 fps, Betri masaa 5:40 (kuzungumza), RAM 512.
Ace: CPU 800 Mhz, Kamera 5MP, Video VGA 15 fps, Betri masaa 6:30 (kuzungumza) RAM 256.
Kwa hiyo Torch inaikaribia simu ya mwisho kabisa katika kumi bora, iwapo wanataka kuingia katika simu bora hawana budi kuwa na viainisho halisi bora zaidi ili kutoa ushindani wa kweli.
Blackberry App World: hii ni aibu ya pili kwa RIM, soko hili la apps lina apps zisizozidi 20,000 ambapo ni chini ya 10% ya appstore ya Apple yenye  apps zaidi ya 200,000 na Android Market yenye apps zaidi ya 150,000. RIM wanalifahamu hili, katika kufanya juhudi za kuwahamasisha watengenezaji wa apps kuingia kwenye soko lao RIM wametoa ahadi ya kumpa zawadi yoyote atakayepeleka app yake kwenye soko lao na kupasishwa, ambapo zawadi yenyewe ni Blackberry Playbook tablet ya bure.
Ni matumaini ya washabiki wa Blackberry na wapenda gajet Ulimwenguni kuwa RIM wamepata funzo kubwa kwenye utengezaji wao wa Blackberry Playbook na udhaifu uliowazi wa simu za Blackaberry. Playbook ni tablet ambayo inatarajiwa kupata mafanikio kwa kuwa imetengenezwa kwa umahiri mkubwa. 


Sisi katika Gajetek tunaamini kwamba  simu ya Blackberry ijayo itaingia katika cha chati yetu ya simu na kukaa kwa muda mrefu. Hata hivyo RIM wafanye haraka kabla ya Blackberry haijageuka kuwa Crapberry.
Advertisements

One thought on “>Kwa Nini Blackberry Haziingii Kwenye 10 Bora?”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s