>Acer Iconia; Laptop ya Aina Yake

>

Skrini 2 za Acer Iconia zinavyoonekana

Laptop hii si mpya, imekuwepo katika Ulimwengu wa Gajet kwa muda wa karibu miezi sita sasa, lakini kinachotufanya kuielezea ni kwamba laptop hii ni tofauti na laptop nyingine zote. Kikubwa kinachoitofautisha ni kuwa na skrini mbili zote za kugusa (touch screens) kila moja ikiwa na ukubwa wa inchi 14, kwa hiyo jumla kwenye laptop hii unapata ukubwa wa inchi 28.

Laptop hii ambayo inatumia Windows 7 haina keyboard wala touchpad halisi bali skrini ya chini huwa na vifaa hivi viwili unapovihitaji, yaani virtual keyboard na virtual touchpad. Kwa wengi wanaona kwamba hili linaipunguza ladha laptop hasa kwa upande wa keyboard kwani kuandika makala ndefu kwenye laptop ya Acer Iconia inakuwa ni kazi kubwa.
Keyboard ya kugusa kwenye skrini ya Acer Iconia
Vile vile skrini ya  chini hubadilika kwa mujibu wa program iliyofunguliwa kwenye skrini ya juu. Kwa mfano utakapofungua program ya Muziki basi skrini ya chini utakuwa na vifungo vya kuwasha kuzima kupeleka mbele, kuriwaindi na kadhalika. 
Laptop hii inatumia gesture kuanzisha propgram mbali mbali, kwa mfano unapoweka vidole kumi kwenye skrini ya chini Iconia hufungua virtual keyboard. Mbali na gestures hizo pia skrini ya chini ambayo hufanya zaidi shughuli ya kuitumia badala kutizamia ina Acer Ring ambayo ina uwezo wa multitouch kwa ajili ya kufanyia mambo mbali mbali katika laptop hiyo ikiwa ni pamoja kutumika kuanzisha mitandao ya kijamii kama vile facebook  na twitter, kuwashia muziki na video, kufungua galari ya picha na kadhalika. Ring hiyo inafunguliwa kwa gesture ya kuweka vidole vitano vyote vya mkono mmoja kwenye skrini. Kompyuta hii pia inakuruhusu kutunga gesture zako mwenyewe kwa mujibu wa mapendekezo binafsi.
Viainisho halisi:
Uzito: Kilo 2.8
Skrini: skrini mbili ambazo ni HD zenye uwezo wa multitouch (mpaka vidole 10)
Ukubwa wa Skrini: Inchi 14 kila moja
Hard Drive:  kuna aina mbili i) 640 GB ii) 750 GB
CPU: Intel Core i5
Kasi ya Prosesa: 2.66 GHz
Vifaa vingine: USB 3.0, HDMI, mikrofoni, inchi 3.5 headphone jack.
Kamera:  Ina 1.3 Megapiksel kwenye skrini ya juu.
OS: Windows 7
RAM: 4 GB
Uzuri: 
Skrini zake ni za hali ya juu na multitouch inafanya kazi kwa ufanisi 
Ni kompyuta ya kujifurahisha (entertainment)
Ina nguvu na kasi ya hali ya juu 
Ina nafasi ya kutosha ya kuhifadhia mafaili
Ubaya: 
Windows 7 si OS ya skrini ya kugusa.
Si kompyuta ya kuandikia makala ndefu. 
Ni nzito mno (Karibu kilo 3)
Ni ghali mno £1,400 (Tsh 3,462,183)
Ushauri:
Hata hivyo kwa ushauri wetu ikiwa unataka laptop ya kufanyia kazi muhimu ambazo zinahitaji kuandika mara kwa mara basi laptop hii haikufai, au ununue keyboard ya kuunganisha, la ikiwa unataka laptop ya kujifurahisha iliyo tofauti basi Acer Iconia itakufaa kwa matumizi yako. Pia laptop hii inafaa kwa kazi ambazo zinahitaji laptop yenye kasi  kama vile video editing.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s