>Operating System za Simu na Tablet (Sehemu 2)

>

Tunaendelea na mfululizo wa makala zetu za OS za simu na tablet na safari hii tutazungumzia iOS ya Apple. OS hii hutumika katika iPod, iPhone na iPad, imeingia ulingoni hasa mwaka 2007 iPhone ilipoanza wakati huo ikijulikana kama iPhone OS, mwaka 2010 ndipo ilipobadilishwa jina na kuitwa iOS.
iOS inavyoonekana katika iPhone 4
Wengi wana mtazamo kwamba hii ni OS bora kuliko zote katika simu na tablet lakini ukweli ni kwamba OS nyingine haziko mbali sana na OS hii, hasa Android, Windows Phone na QNX, pia pamoja na ubora wake ina udhaifu katika nyanja fulani, tuanze kuelezea ubora.
Ubora wa iOS
Ina apps zenye ubora wa hali ya juu kuliko OS nyingine zote kwa vile Apple ni wenye uangalizi mkubwa katika viwango. Kwa sasa apps za iOS ni zaidi ya 200,000. Karibu kila unachofikiria basi utapata app yake ikiwa ni pamoja na app za kufunga, kufungua na kuwasha baadhi ya magari. Hivyo huhitaji ufunguo.Ina apps nyingi kuliko OS zote, kwa vile Apple walikuwa ndio wa mwanzo kuanza utaratibu wa kuwalipa developers (watengenezaji apps) 70% katika mapato ya mauzo ya apps zao na Apple huchukua 30%


Utaratibu wa kuingiza mafaili mbali mbali ya video, picha, muziki, apps, podcast na vitabu (ebooks) ni mzuri kwani huweza kuhamisha moja kwa moja (syncing/synchronising) kutoka kwenye kompyuta kwenda kwenye iPhone, iPod au iPad kwa kutumia iTunes, iTunes huruhusu mpaka kompyuta 5 kwa akaunti moja.
User interface (namna inavyofanya kazi) ina ubora wa hali ya juu, haina kawaida ya kukwama kwama, ni rahisi kutumia na huboreshwa kila baada ya muda mfupi. Ina umri wa miaka chini ya mitano lakini imebadilika mno na kuboreka sana.
Mazungumzo kwa Facetime baina ya iPad 2

Ina huduma ya Facetime, hii ni simu za video baina ya watumiaji wa iOS lakini ni lazima uwe na Wi-Fi, na simu hizo ni bure pia unaweza kumpigia simu hizo mtumiaji wa kompyuta za Apple (iMac, Macbook na Mac Mini) zenye kamera. Hii pia inawezekana tu kwa vifaa vipya vya Apple, yaani iPhone 4, iPad 2 na iPod touch 4.

Udhaifu wa iOS
Hakuna chaguo la simu na Tablet nyingi kwani iOS hii inatumika kwenye simu ya iPhone tu na tablet ya iPad, ambapo Apple hutoa moja tu kila mwaka kwa sasa kuna iPhone nne na iPad mbili tu.
Haikubaliani na website yoyote yenye kutumia flash, hii inaonekana kutokana na vita binafsi vya kibishara kati ya kampuni ya Apple na kampuni ya Adobe wamiliki wa Flash. Pia huenda ikawa ni njia ya Apple kupunguza ushindani kwani kuna game nyingi za flash zilizopo kwenye mtandao. Hata hivyo Apple hutoa hoja kwamba flash haifanyi kazi vizuri kwenye iOS zao na kwamba matatizo mengi ya OSX, operating system ya kompyuta za Apple husababishwa na Flash. Hii huchukuliwa kuwa ni nukta kubwa ya udhaifu wa iOS kwani flash ina washabiki wengi mno kwa vile hutumika kwa video na game katika mitandao mingi Duniani.
Kuna ukiritimba (monopolism) wa hali ya juu kwa vile Apple ni kampuni yenye nguvu mno. Hivyo kila kinachoingizwa huzingatia zaidi manufaa ya Apple, ingawa hii huvunjwa kasi kwani Apple ni kampuni inayoojali wateja.
Simu zake ni ghali mno, kwa mfano iPhone 4 16GB mpya inagharimu £500. (TSh 1,244,724) na hivyo wanaopendelea simu za hali ya chini hawana nafasi ya kuwa nazo katika platfom hii.
iPhone 4
Sehemu ya tatu na ya mwisho ya makala hii tunatarajia kuzungumzia Windows Phone na Symbian OS.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s