>Operating System Za Simu na Tablet (1)

>

Namna ya OS inavyofanya kazi

Operating system ni software yenye programu na data zinazoshugulika na uendeshaji na usawazishaji wa resources mbali mbali katika Kompyuta yoyote. Si kila kompyuta ina operating system. Kwa mfano kompyuta inayoendesha jiko lako la microwave haina operating system kwa vile halina shughuli nyingi za kufanya, kompyuta hii ina programu moja tu ya kuwasha kuzima na kubadili viwango vya moto pamoja na muda. Hata simu za awali kabisa kama vile Nokia Ringo na Motorola Startec ambazo zilikuwa na kazi moja tu ya kupiga simu hazikuwa na haja ya kuwa na operating system.

Kuna operating system nyingi za simu lakin zifuatazo ndio Operating System maarufu zaidi za simu mbali mbali
  1. Android (Google)
  2. iOS (Apple)
  3. Windows Phone (Microsoft)
  4. Symbian (inaendelezwa na Nokia)
  5. QNX (RIM watengenezaji wa Blackberry)
Android
Operating system hii inamilikiwa na kampuni maarufu ya Google. Hii ndio operating system changa kuliko zote ambapo imeanzishwa mwaka 2003 na kununuliwa na Google mwaka 2005. Kwa sasa operating system hii hutumika katika simu na tablet, inayotumika kwenye  simu ni Android Gingerbread 2.3 na tablet ni Android Honeycomb 3.0, ingawa ziko tablet ambazo zinatumia Gingerbread kama vile HTC Flyer na Samsung Galaxy Tab. Inasemekana Android 2.4 Ice cream inakaribia kutolewa ambayo pia itakuwa ni ya simu.
HTC Sensation yenye Android 2.3 Gingerbread

Uzuri wa Android:
Ina uwezo mkubwa wa kutafuta (search engine) nadhani hii ni wazi kwa vile Google ni search engine yenye nguvu na umaarufi mkubwa.

Ni open source: kwa hiyo watumiaji wanaruhusiwa vile vile kuiendeleza na kuigeuza watakavyo, ndio maana utakuta huvalishwa makoti mbali mbali kulingangana na kampuni. Kwa mfano HTC huivalisha koti la HTC Sense, hii hufanya simu zao kuonekana tofauti kidogo na simu nyingine za Android.

Android ina apps (program ndogo ndogo) nyingi za bure  au bei rahisi.

Kuna simu nyingi zitumiazo android lakini maarufu zaidi ni HTC, Samsung, LG, Motorola na Sony Ericsson. Hivyo watumiaji au wapenzi wa android wana nafasi pana ya kuchagua simu waipendayo.

Hupatikana kwenye simu za bei rahisi na simu za ubora wa juu vile vile.

Ina apps nyingi mno, zipatazo laki mbili, kwa sasa ni ya pili baada ya iOS ya Apple kwa idadi ya apps.

Mtumiaji anaweza kuibadili simu kwa kupanga widgets na apps kwa namna inavyompendeza yeye kulingana na matumizi yake.

Motorola Xoom inayotumua Android 3.0 Honeycomb

Ubaya wa Android
Kwa asili, haina uwezo wa kufunga apps na hivyo kufanya apps nyingi ziwe ziko wazi hata kama huzitumii, ingawa kwa sasa kuna apps nyingi ambazo zinafanya kazi ya kufunga apps usizozitumia. Kimsingi hii ilikuwa iwe ni kazi ya operating system badala ya apps.

Nyingi kati ya Apps zake ni za hali ya chini kwa vile ni open source, khii ni kutokana na ukweli kwamba hakuna uangalizi wa ubora wa viwango kwa apps.

Simu za hali ya chini huwa na matatizo mengi na hivyo hufanya kuonekana kama kwamba ni matatizo ya Android, vile vile hii ukosefu wa uangalizi wa ubora wa viwango.

Ingawa kwa sasa imeendelea mno bado haijafikia kiwango cha juu ndio maana kampuni kubwa hujaribu kuibadili ili kuiboresha zaidi ambapo HTC na Samsung wanaonekana kufanikiwa zaidi katika kubadili na kuiboresha. Hata hivyo kwa sasa  Google wanaonekana kujaribu kuliondoa hili kwa kuweka viwango vya hardware hasa katika tablet. Tablet zote zinazotumia Honeycomb ni lazima ziwe na Dual Core Processor na RAM ya chini ni 1GB. Hivi ni viwango vizuri mno kwa tablet na simu.

Makala hii itaendelea na Mungu akipenda sehemu ya pili tutazungumzia iOS ya Apple.
Endelea sehemu ya 2

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s