>NFC: Teknolojia itakayobadili Maisha Duniani

>

Near Field Commnication ni teknolojia ya siku za usoni. Teknolojia hii hujulikana kwa kifupi NFC. Inaitwa ya karibu na field kwa sababu huwa inafanya mawasiliano kwa karibu zaidi hata kuliko bluetooth.
Teknolojia hii tayari inatumika katika simu za mkononi, kwa kawaida inakuwa na pande mbili katika matumizi ambazo huwasiliana. Upande mmoja huanzisha na mwengine hupokea na kurudisha aina fulani ya mawasiliano. Kwa mfano inapotumika kulipia kitu kilichonunuliwa, simu yenye NFC hutoa taarifa za akaunti ya benki kuipa mashine ya kulipia yenye kisoma NFC (NFC  reader) mashine ya kulipia hupokea taarifa za akaunti ya mlipaji na kutoza kiasi cha fedha alizotumia.

Teknolojia hii huweza kuifanya simu kupashana taarifa mbali mbali na vyombo vingine ikiwa ni pamoja na kuwasiliana kwa kubadilishana tarakimu, kusoma taarifa zilizomo kwenye card za electroniki, kuwasiliana taarifa za barcode, stickers, tags na funguo aina ya fobs. Pia huweza kufanya mawasiliano ambayo hufanywa kwa teknolojia ya bluetooth kwa ufanisi zaidi kwa watumiaji kubadilisha taarifa na mafaili mbali mbali.

Kwa hiyo kwa kupitia teknolojia ya NFC simu inaweza kutumika kununulia bidhaa madukani, kufungua mlango, kuwasha gari, kuazima vitabu maktaba, kujaliza fedha kwenye simu, kulipa bili, kulipa tiketi za treni au basi, kuingilia sinema na kadhalika. Kwa kifupi teknolojia hii itamuondolea mwanadamu ulazima wa kuwa na vyote ambavyo vinakaa kwenye walet au kipochi.

Funguo aina ya Fob ya BMW ikifanya malipo 
kwenye mashine ya kulipia
Teknolojia hii ina usalama wa hali ya juu kwani iwapo utapoteza simu yako mtu atakayeokota hataweza kufanya chochote kwa kutumia NFC. Teknolojia hii tayari inatumika kufanyia mambo haya na watu wasiopungua milioni nne na nusu Duniani kote na hasa Bara la Ulaya na Amerika ya Kaskazini na Asia. Japan ndio inayoongoza kwa kuwa na watumiaji wengi zaidi. NFC pia tayari inatumika katika nchi zinazoendelea, kwa mfano kampuni ya Geti nchini Morocco inafanya mawasiliano mbali mbali kwa kutumia NFC.
Simu ambazo tayari zina teknolojia hii ni pamoja na Google Nexus S, Nokia C7, Samsung Galaxy SII, Blackberry torch na nyinginezo. Hata hivyo Google Nexus S ina kisoma NFC (NFC reader) badala kuwa ni kianzilishi (initiator) Kwa kifupi teknolojia hii iko tayari lakini inahitaji kukubalika zaidi na watumiaji kabla utumiaji wake kuwa ni jambo la kawaida. Hata hivyo kampuni ya Apple ambayo inatengeneza iPhone imekaa kimnya kuhusu teknolojia hii, bado haijaunga mkono wala kusema lolote. 

Ingawa kampuni ya Geti ya Morocco imeweza kuingiza Teknolojia hii katika iPhone, Apple bado ni kiungo muhimu ili teknolojia hii iweze kutumika na kusambaa kwa haraka zaidi. Si jambo kubwa kwa simu kuingizwa teknolojia hiyo kwani hata simu tunazoziita “vimeo” zina uwezo wa kuwa na teknolojia ya NFC, lakini kampuni kubwa kama Apple ni lazima ziiunge mkono.

Hata hivyo teknolojia hii inaweza kutumika kwenye vyombo mbali mbali na si lazima kuwa ni simu ya mkononi.
Advertisements

2 thoughts on “>NFC: Teknolojia itakayobadili Maisha Duniani”

  1. >Du!! hii ni kibokoKwakweli Teknolojia hii inarahisisha mambo mengi sana,na itatusaidia sana iwapo itaenea kwa wingi ktk ulimwengu wetu wa tatu.

  2. >haya ndio mambo tunayotakiwa binaadamu kuyafanya kujaribu kurahisisha na sio kugumisha maisha.hongera kwa mvumbuzi na pia hongera kwako ulietujulisha maendeleo haya.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s