>Uzinduzi Rasmi wa Gajetek

>

G ndio herufi, haiwakilishi Gangsta wala Google bali ni alama rasmi ya blogi mpya iinayojulikana kama GAJETEK. Lengo kuu katika blogi hii ni kuwapa habari na kuwaelemisha wazungumzaji wa lugha ya kiswahili juu ya masuala ya Gajeti na Teknolojia. Tunachukua nafasi kuwakaribisha wasomaji na wapenzi wa gajet katika blogi yetu, ni matumaini yetu kuwa mtaburudika na kuelemika na makala na habari mbali mbali tulizoandika na tutakazoandika.
G kubwa,  alama ya Gajetek, blogi mpya wa 
Gajeti na TeknolojiaNi wazi kuwa tunakabiliwa na changamoto kubwa kwa vile lugha ya masuala ya gajeti  bado ni changa katika Kiswahili. Tunaamini kuwa Gajetek ni blogi ya kwanza ya kiswahili ambayo ina muelekeo huu. Hivyo basi tutaazima na kulazimisha maneno katika matumizi. Kwa mfano Gygabite tutaiiita gigabayt, kwa sasa hatuna njia nyingine.


Tungependa kuwajulisha wasomaji wote kuwa blogi hii haina mfungamano wala uhusiano na kampuni au blogi yoyote inayohusiana na gajet, hivyo basi tunaamini kuwa hii itatuwezesha kuandika habari huru zisizo na upendeleo wala mfungamano na kampuni yoyote, tofauti na kampuni zenyewe ambapo wanapotoa bidhaa huwa zao wanazielezea kwa lengo la kuzitangaza tu.
 Gajetek itakuwa inaandika habari zinazohusu mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kompyuta, magari, ndege, simu, programu, kamera, TV pamoja na wataalam mbali mbali katika fani ya teknolojia. Usisite kutuandikia kwa ajili ya ushauri au jambo lolote kwa anuani gajetek@gajetek.com Kublogi kwetu ni fani na tungependa kwa wasomaji wetu iwe ni burudani. Leo tarehe 20/05/2011 ni tarehe ya kuzaliwa kwa Gajetek na tunamuomba Mola aipe baraka zake ili iweze kutoa manufaa kwa wasomaji. 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s