>Microsoft Wainunua Skype

>

Nembo ya Skype, kampuni yenye kutoa huduma ya
kuchat na simu za mtandao
Afisa mtendaji mkuu wa Microsoft, Steve Ballmer amethibitisha kwamba Microsoft imeinunua Skype. Skype ambayo ni kampuni ya simu za mtandao ina watumiaji wapatao milioni 663 duniani kote. Skype imeigharimu Microsoft $ 8.5 bilioni. Bei hiyo inaonekana ni kubwa mno kwa vile mwaka 2006 kampuni ya mnada wa mtandaoni, eBay iliinunua kampuni hiyo kwa $ 2.6 bilioni. Mwaka 2009 eBay waliuza 70% ya hisa za Skype kwa $2 bilioni. 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Microsoft, Steve Ballmer (Kushoto)
akiwa na mwanzilishi wa Microsoft Bill  Gates
Wachambuzi wanaamini kwamba Microsoft wanaihitaji skype hasa ukizingatia kwamba kampuni hiyo iko njiani kutoa OS ya tableti ambayo inatarajiwa kuitwa Windows 8. Vile vile ununuzi huu ni kujihami kwa Microsoft kwa vile simu, kompyuta pamoja na tableti za Apple ni zenye kutumia huduma ya Facetime ambayo kwa namna fulani ni sawa na skype, yaani ina uwezo wa kupiga simu za video, ingawa skype ni maarufu zaidi kwa vile inatumika kwenye platfomu mbali mbali ikiwa ni pamoja na Windows, Windows Phone, iOS (iPad, iPhone na iPod) na Android (simu na tableti)
Microsoft imeeleza kwamba Tony Bates ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Skype ataendelea kushikilia nafasi yake wakati Skype inakuwa ni kitengo kinachojitegemea ndani ya Microsoft. Colins Gillis mchambuzi wa BGC Finacial ameelezea kuwa ununuzi huu kwa Microsoft ni mkakati na kujihami utakaowasaidia sana katika OS ya tableti, Windows 8. 
Wengi wanahoji juu ya uhalali wa bei kubwa ambayo Microsoft wamenunulia Skype ambayo hupiga simu na simu za video bure baina ya watumiaji wa skype na hugharimu fedha kidogo tu kupiga simu kwenye simu za mkononi na nyumbani. Skype ilianzishwa mwaka 2003.
Je ni mkakati gani ambao wataufanya Microsoft ukizingatia wapinzani wakubwa wao kibiashara katika simu, tableti na Kompyuta yaani Apple na Android ni zenye kutumia skype. Iwapo wataamua kuitoa skype katika platfomu hizo maana yake ni kupunguza watumiaji. Iwapo wataamua kuwa watumiaji wa Apple na Android waendelee kutumia skype ni wazi kwamba Micrsoft haitapata manufaa zaidi kuliko wapinzani wao. Ni lazima Microsoft wawe makini katika maamuzi yao. 
Advertisements

2 thoughts on “>Microsoft Wainunua Skype”

  1. >Jee sasa hiyo skype wameondoa ile huduma ya bure ya video call?Juzi niliona program ya ku update skype ambayo niliulizwa na laptop yangu. Baada ya kuclick ýes sasa ile huduma ya video call inaonyesha haiko active na inajipeleka kwenye phone call.Nimeishiwa nguvu kabisa.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s