>Blackberry Playbook matatani?

>

Blackberry Playbook, tablet ya RIM

Vita vya kibiashara katika uwanja wa tablet sasa vimepamba moto, RIM watengenezaji wa simu za Blackberry ambazo zimepata umaarufu mkubwa kutokana na kuwepo kwa huduma maarufu ya ujumbe inayojulikana kama BBM na OS ya aina yake wameingia ulingoni na Blackberry Playbook. 
Wakati wengi wamekuwa wakiisubiri kwa hamu, RIM kampuni iliyotengeneza Blackberry playbook tayari imeomba kurudishwa kiwandani kwa ajili marekebisho tableti zipatazo 1000 na kusema kwamba OS ina matatizo. hata hivyo ni wazi kuwa RIM inegundua suluhisho la matatizo ya tablet hiyo ambapo zitakazotoka Barani ulayo mwezi wa June zitakuwa hazina tatizo hilo. Hii huenda ikaathiri mauzo kwa vile wengi huenda wakaghairi kununua wakisikilizia habari za tatizo hili.

Vianisho halisi vya Blackberry Playbook vinaonesha kwamba tablet hii ni miongoni mwa tablet zenye nguvu na kasi sana kama ifuatavyo:

  • Kiendesha (Operating Ssystem): Blackberry
  • Kumbukumbu (RAM): 1GB
  • Prosesa ya kati (CPU): Dual Core (1Ghz)
  • Skrini: 7” ikiwa na rizolushan 1024×600 
  • Kamera: ya mbele ni  mega piksel 3 na ya nyuma  mega piksel 5
  • Kurekodi video: HD 1080p kamili kwa kamera ya nyuma
  • Nafasi ya disk: aina tatu – ama 16GB au 32GB au 64GB
Vipimo vya Blackberry Playbook

Huko Marekani bei ya Blackberry Playbook ni sawa na iPad 2. Wakati huko tayari zimeanza kuuzwa kampuni za Carphonewarehouse, Phones4U na nyinginezo zimetangaza kuanza mauzo tarehe 15 mwezi Juni nchini Uingereza. Pia bara zima la Ulaya litaanza mauzo ya tablet hiyo mwezi wa Juni.

Wakati kila kila kianisho halisi kinaonesha kwamba Blackberry playbook ni tablet yenye kasi na nguvu wengi wameona kinachorejesha nyuma kuhusu tableti hii ni ukosefu ya apps nyingi katika soko la programu za tablet hii. Hii huenda imechangiwa sana na ukweli kwamba RIM wamechelewa mno kuingia kwenye uwanja wa tablet ukizingatia kwamba OS tatu kwa sasa tayari zinaendesha tablet ikiwa ni pamoja na iOS ya Apple, Android ya Google na Windows 7 ya Microsoft (Windows), ingawa Windows 7 imekuwa ikikosolowe sana kuwa haiko tayari kwa tablet jambo ambalo limewafanya windows kuanza kuipika Windows 8 ambayo nayo itakuwa ni maalum kwa tablet.
Je Blackberry playbook itaweza kutoa upinzani wa kweli kwa iPad 2? Suali hili ni gumu lakini ni wazi kwamba wateja wataweza kuwa na chaguo tofauti mbali na utitiri wa tablet za Android,  iwapo wamechoshwa au hawapendelei kutumia iPad. 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s