>Cheza game kwa akili tu!

>

Sasa tuelekee kwenye ulimwengu wa kesho kabla kesho haijafika. Kampuni ya Neurosky imetengeneza vipaza sauti vya kubana kichwa (headsets/headphones) ambavyo vina uwezo wa kuyafasiri na kuyafahamu mawimbi ya akili na hivyo kumfanya mtumiaji aweze kufanya mawasiliano bila ya kutumia kiungo chochote cha mwili zaidi ya akili. Yaani tunamaanisha headset hizi zina uwezo wa kujua unachokifikiria kwa hiyo mtumiaji anaweza kucheza michezo ya kompyuta (computer games) kwa kutumia akili tu bila ya kushika au kufanya chochote.

Wengi walishangazwa na kufurahishwa na kifaa cha XBox kiitwacho kinect na kudhani kwamba kinect ndio mwisho wa njia kwa vile wacheza game za Xbox hutumia miili yao kushiriki katika michezo hiyo badala ya kontrola. Hili inatufanya tuhisi kwamba inakokwenda teknolojia na maendeleo ya sayansi ni balaa. headset hii itawasaidia  walemavu wa mikono kuweza  kushiriki katika michezo ya kompyuta.
Kifaa hichi ambacho kina kisoma hisia (sensor) kinachokaa kwenye kipaji cha uso huweza kufahamu hisia mbali mbali kama vile kushtuka, kufurahi, kuwa makini, kuwa na utulivu na kadhalika, hisia hizi zote zipo kwenye sehemu ya ubongo ijulikanayo kama pre frontal cortex, hizi ambazo ndizo mwanadamu hizitumia kutoa maamuzi mbali mbali katika kufanya mambo. Kwa kifupi kifaa hichi kina uwezo wa kuwasiliana na mawimbi ya akili inapofanya maamuzi au kuwaza jambo.
Wataalamu wa Neurosky bado wamo katika kufanya utafiti juu ya namna kifaa hichi kitakavyoweza kutumika katika shughuli mbali mbali za maisha ya kila siku ya binadamu. Kifaa hichi tayari kimeanza kuuzwa kwa £99 sawa na TSh, 243,604, ukilinganisha na bei ya headset za Beats By Dre ambazo nyingine huuzwa kwa £279 (TSh. 686,000) tunaweza kusema kwamba bei hii ni ya ubwete. 
Kwa mujibu wa wataalam wa Neurosky game za kifaa hichi zimetengenezwa kwa lengo la kusaidia akili kufanya kazi zaidi na hivyo kupanua uwezo wa kiakili wa mwenye kucheza. Game ambayo inatumika kwenye Kompyuta za aina ya Mac iijulikanayo kama Brainwave Visualiser ni miongoni mwa game hizo. Game nyingine ni Alchemy visualiser. Pia game za kifaa hichi tayari zinapatikana katika iPad, iPhone na iPod Touch. Mfano ni Bullet Dodger ambayo ni game unacheza na kujaribu kukwepa risasi kwa kufukiria tu, kwa uwapo utachelea kufukiri  risasi itakuwa imekupata na hivyo game hii humsaidia mchezaji kujifunza kufikiri kwa haraka.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s