>Samsung yashusha laptop nyembamba Duniani!

>

Samsung 9 Series, nyembamba
mno na nyepesi mno.
Kama unataka kununua laptop na unachojali ni wepesi, ubora, yenye Windows 7 na bei si tatizo basi laptop ya Samsung 9 Series yaweza kuwa chaguo lako. Laptop hii ambayo ina skrini ya nchi 13.3” ambayo inatumia teknolojia ya Super bright plus  yenye kun’gara kwa hali ya juu na kutoa picha iliyo safi mno.


Vile vile laptop hii ina specs zifuatazo:-
CPU: Kizazi cha pili cha Intel® CoreTM i5 Processor 2537M (1.40 GHz, 3MB) 
Inaendeshwa na: Genuine Windows® 7 Home Premium (64 bit) / Windows® 7 Professional (64 bit) 
RAM: 4GB DDR3 
Nafasi ya kuhifadhi mafaili: (max): 128GB aina ya Solid State Drive (SSD) 
Skrini: 13.3-inch HD LED-backlit SuperBright Plus display (400 nit) 
Resolution: 1366×768 
Graphics: Intel HD GT2 Integrated Graphics 
Spika: 3 watt (1.5W x 2) stereo speakers and 1.5 watt sub-woofer 
Batri: Lithium Polymer; up to 6.5 hours 
Mitandao: 802.11b/g/n; WiMaxi 
Uzito: 2.89 lbs.
Kinachovutia zaidi ni ubora na wembamba wa laptop hii. Ina upana wa 16mm na uzito wa kilo 1.3, ukizingatia macbook air ina upana wa 17mm, Samsung wameshusha kitu chenye kuvutia mno. Hata hivyo chenye kuvunja moyo ni ambapo kwa sasa inauzwa £1,300 sawa na Tsh , 2,000,000 hata hivyo kama tunavyojua kuwa siku zote vizuri huwa ghali. Pia laptop hii ina bluetooth 3.0 na USB 3.0 zenye uwezo mkubwa wa kuhamisha data kwa kasi ya hali ya juu. 
Akizungumza kuhusu laptop huu Mkurugenzi ya Kompyuta ndogo (Mobile Computers) kitengo cha Masoko Samsung Bwana Scott Ledterman amesema “tulipoibuni na kuitengeneza Kompyuta hii tulitaka wateja wetu wawe na uzoefu ambao hawataisahau Kompyuta hii kwani ni ya namna ya pekee, ina nguvu katika ufanyaji kazi wake, ni nyembamba na nyepesi.”

Malighafi iliyotumika katika utengeneza wa gamba la kompyuta lenye mvuto wa aina yake ni Duralumin ambayo hutumika katika ujenzi wa ndege yenye umadhibuti mara mbili ya aluminium. 

Advertisements

2 thoughts on “>Samsung yashusha laptop nyembamba Duniani!”

  1. >sijawahi hata kufikiria kitu kama hichi kinawezekana hii iko juu vibaya vibaya hongereni sana hapa mmmevumbua kitu cha ukweli.na naona nafikiria kuinunua.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s