>Uvumi Kuhusu iPhone 5 Wazidi Kusambaa

>

iPhone 5, simu inayosubiriwa kwa hamu na washabiki wa Apple imeendelea kuvuma katika ulimwengu wa gajeti, kukiwa na madai kemkem juu ya namna iPhone hiyo ilivyobadilika ikilinganishwa na iPhone 4. Badiliko kubwa ni uvumi kwamba iPhone hiyo itakuwa na skrini yenye ukubwa wa 4” badala ya 3.5 kama zilivyo iPhone zote zilizotangulia. Katika uzinduzi wa iPhone 4 Steve Jobs aliwahi kudai kwamba skrini kubwa zaidi ya 3.5” si kitu ambacho Apple hawatarajii kukifanya kwa vile ukubwa huo utazidi kiasi ambacho simu inatakiwa iwe.
Je hii ni iPhone 5 ya kweli au ni mambo ya photoshop tu?
Vile vile uvumi mwingine kuhusu iPhone 5 hiyo ni kwamba Apple wataachana na umbile la iPhone 4 na hivyo simu mpya hiyo itafanana zaidi na iPod touch 4 au iPad 2. Kwa kawaida Apple ni wasiri mno na hivyo huzuia habari zote za bidhaa zao kabla ya uzinduzi rasmi, hivyo kabla ya uzinduzi huo ambao kwa kawaida hufanyika mnamo mwezi wa Juni, iPhone hii itabaki kuwa ni uvumi tu. Hata hivyo mapaparazi wa Gizmodo katika uwanja wa gajeti waliwahi kuivujisha iPhone 4 hata kabla ya Apple kuitangaza. 

Ukweli wa mambo utajulikana hivi karibuni ingawa wako wanaodai kwamba mwaka huu Apple watachelewesha simu hiyo badala ya kutoka mwezi wa June itatoka mwezi wa tisa. Aijue siri hii kiukweli ni Steve Jobs na wenziwe.
Advertisements

One thought on “>Uvumi Kuhusu iPhone 5 Wazidi Kusambaa”

  1. >kwa ukubwa huo unaotarajiwa kwa maoni yangu hii haitokuwa simu tena. mi naona wajaribu kutengeneza kitu kidogo rahisi kuchukulika na pia chenye teknolojia ya juu kama hivyo kitakua kizuri pia hata kiusalama

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s