>Samsung Galaxy S II kiboko ya iPhone 4?

>

Samsung Galaxy SII
Je hatimae iPhone 4 imepata kiboko yake? iPhone 4 imekuwa ulingoni karibu mwaka mmoja sasa, lakini simu hiyo bado imekuwa juu ya chati zote za simu. Hata hivyo hili huenda sasa limefikia ukingoni kwani Galaxy S II imeteremka na vianisho halisi (specification) sio vya kawaida. Simu hiyo yenye Dual core processor yenye kasi ya 1.2Ghz, ina kamera yenye uwezo wa kurikodi video ya HD 1080p kamili, pia kamera hiyo ina 8mp ambapo iPhone 4 hurikodi video za 720p na picha 5mp tu. 

Steve Jobs alijigamba sana wakati iPhone 4 inatoka kuwa ni simu nyembamba kuliko zone duniani, Hilo si kweli tena kwani Galazy S II in a wembamba wa 8.49mm na kuifanya kuwa ni simu nyembamba kuliko zone Duniani.

Ikiwa na skrini aina ya super Amoled plus yenye mng’aro wa aina yake, ukubwa wa skrini ya Galaxy S II ni 4.3″ na kuizidi iPhone kwa 0.7″, hata hivyo mng’aro wa skrini ya iPhone yenye 320ppi ni kuliko uwezo wa jicho kuona, kwani jicho huona 300ppi tu.
Samsung wanajitapa zaidi kwamba simu hiyo ina uwezo wa kutuma ujumbe mfupi kwa kutumia sauti badala ya kuandika, hii itawasaidia sana wale wenye kutuma ujumbe huku wakiendesha gari kwa mfano. Hata hivyo kazi itakupata iwapo utataka kutuma ujumbe huo kwa lugha ya Kiswahili, kwani “voice recognition” ya Google haifahamu lugha hii. Simu hii inatumia Android Gingerbread ambayo ndio OS mpya ya Google.

Tusisahau pia iPhone inabaki kuwa kinara kwa kuwa na Apps nyingi na bora zaidi kuliko zile za Android na pia kwa wale washabiki wa Apple wanadhani kwamba Android kama OS bado haijaifikia iOS ya iPhone.


Pia Samsung Galaxy SII ina uwezo wa kudawnlod data katika kasi ya 21mbps kwa sasa ndio simu yenye kasi zaidi. Je ni kweli simu hii imeipiku iPhone 4? Hili ni Swali gumu kulijibu kwa vile zimetoka simu nyingi na katika mwezi au wiki ya mwanzo wachambuzi wa gajeti wamezipa sifa hiyo lakini muda mchache baadae iPhone 4 inarejea kinarani. Lakini iwapo utawauliza washabiki wa Android bila shaka watakuthibitishia kwamba simu hii ni kiboko ya iPhone 4.

Advertisements

2 thoughts on “>Samsung Galaxy S II kiboko ya iPhone 4?”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s