>Beru Factor 001: Baskeli ya TSh 52,000,000!

>

Beru Factor 001 = Tsh 52,000,000.00
Yap, hatujakosea idadi ya sifuri, ni Shilingi milioni 52 za Kitanzania, unaweza kujenga nyumba ya vyumba 3 au 4 au kufungua duka zima la baskeli au ukanunua BMW 1 Series mpya kabisa na kubakiwa na chenji kama ya milioni 8 hivi, lakini kwa baskeli aina ya Beru factor 001, unapata baskeli moja tu,  tuachane na bei na kuzungumzia vikorokoro katika baskeli hiyo.
Baskeli hii imetengenezwa na wataalam wa Formula 1 wakishirikiana na Chuo kikuu cha Lughborough cha Uingereza. Chuo kikuu cha Loughborough ni chuo kikuu bora katika michezo nchini Uingereza kwa zaidi wa miaka 20 mfululizo. 


Fremu ya Beru Factor 001 imetengenezwa kwa malighafi aina ya carbon fibre monocoque ambayo hutumika kutengenezea gari za Formula 1, malighafi hii inaifanya baskeli kuwa na umadhubuti wa hali juu na uzito mdogo sana. Bila ya kutia chumvi unaweza kuinyanyua baskeli hii kwa kidole kimoja tu lakini hautaweza kuipinda hata ukiamua kuigonga kwa nyundo nzito! kikubwa utachuna rangi tu.

Ni wazi kuwa baskeli hii imetengezwa 
kwa utaalamu wa hali ya juu!

Baskeli hii ina kompyuta yenye skrini ya kugusa (touch screen) ambayo inakupa taarifa kama vile kasi uendayo, mahala ulipo (GPS), joto la mwili kwa kutumia bluetooth iliyounganishwa na kifaa unachotakiwa kukivaa, joto la mazingira kwa kutumia kipima joto na undeshaji wako wa baskeli hiyo, kwa mfano kompyuta hii unaweza kukujulisha kama unatumia nguvu zaidi kwa mguu wa kulia kuliko wa kushoto, taarifa hii kwa mimi na wewe inaweza kuwa haina maana yoyote lakini kwa washindanaji baskeli ni taarifa muhimu mno.


Wanunuaji wa baskeli hiyo hutengenezewa kwa mujibu ya maumbile na uwezo wao wa kuendesha baskeli. Mteja hutakiwa kwenda maabara za Chuo kikuu cha Loughbough kufanyiwa uchunguzi wa afya na maumbile ili atengenezewe baskeli hiyo. Wataalam sita huchukua muda wa wiki nzima kukamilisha utengenezaji. Baiskeli hiyo tayari umeshawekwa katika makumbusho ya kisayansi nchini Uingereza kutokana na ubora wake.


Baskeli hii ambayo ni kitu muhimu kwa washindanaji katika mchezo wa kuendesha baskeli ina breki maalum zinazotumia haidroliki badala ya breki za kawaida za baskeli, pia ina gia ya umeme iwapo unataka kwenda mwendo wa gari kama Lance Amstrong, yaani 80 kph.

Hii ni baskeli ya mazoezi kwa washindanaji ambayo ili uweze kununua ni lazima uwe mtoto wa milionea au milionea mtoto, vinginevyo uwe kwenye timu kama vile Team GB Cycling, na umeshatengeneza fedha kwa kushinda medali kadhaa. 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s