>Vimbwanga vya Ford Focus mpya

>


Ford Focus 2011

Hii si Baghatti Veryon wala si Ferrari, ni gari ya kawaida tu hata hivyo imeshushwa na vijimambo ambavyo huvitarajii kwenye gari kama hii. Gari imetengenezwa kwa ajili ya kurahisisha maisha kwa wale wanaoishi katika miji mikubwa kama Vile New York, London Paris, Dar es Salaam, Nairobi na kwengine kokote duniani ambako kuna msomgamano wa magari na matatizo mbali mbali yanayohusiana na uendeshaji wa gari, ambao ni matokeo ya ukubwa wa miji hiyo.Kwa wale ambao wanaishi katika miji hii ambayo nafasi ya kuegesha gari ni tatizo, tulieni, Ford Focus hii ina teknolojia ya kujiendesha wenyewe na kujiegesha katika mtindo wa uegeshaji sambamba (parallel parking) bila ya dereva kufanya lolote, hivyo basi hutoa msaada mkubwa hasa pale sehemu ya kuegeshea inapokuwa imebanwa, anachohitaji kufanya dereva ni kuweka sambamba na gari ya mbele ya nafasi ya kuegesha na kubonyeza kifungo cha kuegesha, halafu anaweza kuanza kunywa soda wakati gari inajiegesha wenyewe.
Ford Focus ikijiegesha yenyewe katika “parallel parking”
Vilevile gari hii ambayo imefungwa kamera yenye utaalam wa robot sehemu ya mbele; iwapo dereva atachelewa kupiga breki basi Ford Focus husimama wenyewe inapogundua kwamba kuna kitu mbele au gari ya mbele imesimama ghafla na hivyo huweza kuepusha ajali iwapo gari haiendi kwa kasi kubwa.
Focus ina uwezo wa kujipiga breki iwapo kuna kitu chochote mbele yake na hivyo kuwa na uwezo wa kuepusha ajali katika mwendo mdogo
Kwa wale wanaoendesha kwenye barabara zenye lane (mistari ya barabara) nyingi, Ford Focus pia inatumia kamera zake kuhakikisha kwamba gari inabaki ndani ya lane yake, yaani kila inapogusa mstari, gari hurudishwa.
Ford Focus inauwezo wa kutoa msaada kwa dereva ili kuhakikisha
gari haitoki kwenye mstari wake

Ford Focus hii pia ina shuttters maalum ambazo hujifunga na kujifungua ili kubana matumizi ya mafuta ya gari kwa kuruhu na kuzuia msukumano (resistance) wa upepo. Gari hii pia ina bluetooth kwa ajili ya simu na vifaa vingine, DAB radio, Cruise Control, hutoa taarifa kwa dereva kwa kutumia kompyta iwapo upepo utapungua kwenye matairi na ina uwezo wa kusoma alama za barabarani kama vile spidi inayoruhusiwa, alama ya kusimama na kuzionesha alama hizo kwenye kompyuta ya dashibodi.
Advertisements

One thought on “>Vimbwanga vya Ford Focus mpya”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s