>iSteve: Kitabu cha Jobs

>

Steve Jobs katika uzinduzi wa iPad 2 Cupertino, 
Carlifonia makao makuu ya Apple yaliyopo 

iSteve: the Book of Jobs ndio jina ambalo limepewa tarijama (autobiography) rasmi ya Steve Jobs, Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kampuni ya Apple ambapo makubaliano ya kuiandika yamefikiwa. Jina hili limeanzia herufi “i” kwa vile bidhaa nyingi za Apple huanzia herufi hiyo ikiwa ni pamoja na iPad, iPhone, iPod na iMac. 


Kitabu hicho kinachotarajiwa kutolewa mapema mwakani kitaandikwa na mwandishi maarufu Walter Isaacson.  Mwandishi gwiji yuhu ambaye kwa sasa ni Rais wa CNN na Jarida la Time pia ameandika tarijama za Benjamin Franklin na  Albert Einstein, vitabu ambavyo vimepata mafanikio ya hali ya juu katika mauzo.

Makubaliano ya kuandika tarijama ya Steve Jobs yamekuja baada ya kutokuwepo kwa makubaliano kwa zaidi ya miaka mitatu. Mzozo huo ulihusiana na nini kiwemo katika kitabu hicho kuhusu ya maisha yake binafsi pamoja na namna ya kuwagawana mapato yatakayotokana na mauzo ya tarijama hiyo.
Steve Jobs ambaye yupo katika likizo ya kuumwa amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa katika pancreas kwa muda mrefu sasa kiasi kwamba kuna wingu limetanda juu ya kuwepo au kutokuwepo kwake katika uzinduzi ujao wa bidhaa mpya za Apple. Uzinduzi huo unatarajia pia kutangazwa kwa iPhone 5 au iPhone Nano kwa mujibu wa uvumi uliosambaa katika ulimwengu wa gajeti. Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika mwezi wa Juni mwaka huu.
Wengi wanaamini kwamba mafanikio makubwa ya kampuni ya Apple yametokana na ujuzi na ubunifu mkubwa wa Steve Jobs na kufanya mauzo katika kampuni hiyo kukua kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 100% na faida kuongezeka kwa 90%. Kampuni hiyo imepata mafanikio makubwa zaidi katika bidhaa mbali mbali na hasa iPod, iPhone na iPad. Ingawa kuna tarijama nyingi ambazo zimeandikwa kuhusu Steve Jobs, “iSteve: The Book Of Jobs” itakuwa ni tarijama ya kwanza rasmi iliyopata baraka zake mwenyewe.
Advertisements

One thought on “>iSteve: Kitabu cha Jobs”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s