>HTC Flyer yaingia madukani Ulaya

>

HTC Flyer yenye Android Gingerbread 2.3 
iliyovalishwa koti la HTC Sense UI.
Bila ya shaka HTC wamepata mafanikio makubwa katika simu kutokana na ubora wa hali ya juu wa simu hizo. Sasa HTC imeingia katika ulingo wa tableti kwa mtindo wa aina yao peke yao. Kinachoitofautisha tableti hii iliyopewa jina la Flyer ni teknolojia maalum inayoiwezesha peni ya aina yake kuandika katika tableti hiyo. Tableti hii wiki imeingia katika maduka mbali mbali nchini Uingereza pamoja na bara zima la Ulaya wiki hii. 

HTC Flyer imeingia na vianisho halisi (specification) sio vya kitoto, ikiendeshwa na Android Gingerbread 2.3, na CPU yenye kasi ya 1.5Ghz aina ya Qualcomm snapdragon, HD Kamera (Nyuma) na Kamera nyingine mbele pamoja na skrini ya kugusa 7” aina ya LCD. 


Kinachoifanya tableti hiyo  kuwa si kama utitiri wa tableti nyingine na kutofautiana nazo ni peni maalum yenye HTC scribe Technology pamoja na kuivalisha koti Android  Gingerbread kwa kuingiza HTC Sense UI. Peni hiyo inaweza kumruhusu mtumiaji kuandika katika tableti bila ya matatizo yoyote. Kama tunavyojua ni vigumu kuandikia vidole katika skrini za kugusa.

Wakati jina la HTC linatosha kuifanya tableti hii kupata mauzo wachambuzi katika fani ya gajeti wamekuwa wakijiuliza ni vipi HTC wataweza kupata mafanikio katika mauzo kwa sababu zifutazo:-
Wametumia Android Ginbgerdread 2.3 au 2.4 ambayo ni maalum kwa simu badala ya Honeycomb 3.0 ambayo ni Android maalum ya kompyuta za tablet wakati tayari kwenye soko kuna Motorola Zoom na Acer Iconia Tableti zote zimesimikwa na Honeycomb. HTC hawakuainisha kwamba hapo baadae kuipandisha daraja na kuwa na honeycomb. Vile vile tableti hiyo ni ghali kuliko mfalme wa sasa wa tableti zote yaani iPad 2. Wakati 16GB, Wifi na 3G ipad 2 inauzwa £599.00 na 32GB, wifi na 3G ni 579.00. HTC flyer inauzwa kwa bei ya £579.99 kwa 16GB na £599.99 kwa 32GB ikiwa ina bei kubwa zaidi ya Apple iPad 2. Je kuwa na uwezo wa kupakia Flash web inatosha kuwafanya watu waache iPad 2 na kununua HTC flyer? Majibu yatatoka pale HTC itakapotangazo mauzo ya robo ya tatu ya mwaka katika kipindi cha Septemba mwaka huu na hasa tukizingatia kwamba Acer Iconia na Motorola Zoom zinauzwa bei rahisi kuliko HTC Flyer.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s